'UPELELEZI WA KESI YA UGAIDI DAR HAUJAKAMILIKA'

Upande wa  mashtaka umeomba kuongezewa muda wa kukamilisha upelelezi katika kesi ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi inayokabili watu 17.
Wakili wa Serikali, Peter Njike alidai mahakamani mbele ya  Hakimu Hellen Riwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwamba kwa sasa upelelezi haujakamilika.
Hakimu  alikubali ombi  hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6 mwaka huu. Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 17 mwaka huu.
Katika kesi  hiyo, washitakiwa wanadaiwa katika tarehe tofauti nchini kati ya Januari mwaka jana na Juni  mwaka huu,  walipanga njama za kutenda kosa la kuwaingiza watu nchini kwa ajili ya kufanya vitendo vya ugaidi.
Ilidaiwa katika kipindi hicho, washitakiwa  inadaiwa walikubali kuingiza nchini, Sadick Absaloum na Farah Omary  kujihusisha na vitendo vya ugaidi.

No comments: