PINDA MGENI RASMI BARAZA LA IDDI EL FITRI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Idd-el-Fitri litakalofanyika katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Suleiman Lolila baraza hilo litaanza saa 10.00 alasiri ikiwa ni sikukuu hiyo itaadhimishwa kitaifa katika mkoa wa Dar es Salaam.
Lolila alisema sikukuu ya Idd-el-Fitri inatarajiwa kuwa kati ya Jumatatu na Jumanne ya wiki ijayo kulingana na mwandamo wa mwezi na swala yake itaswaliwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1.30 asubuhi.

No comments: