Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam
imeweka kibano kwa watu wenye mavazi yasiyo na staha kuingia makahamani hapo
kwa kuwazuia mlangoni.
Miongoni
mwa mavazi ambayo akivaa mtu anazuiwa kuingia si tu ndani ya vyumba vya
Mahakama, bali pia kwenye viwanja vyake, ni yanayobana, yanayoacha mgongo wazi,
fupi na mashati au blauzi za mikono mifupi.
Hatua
hiyo ilianza kutekelezwa takribani wiki tatu zilizopita. Kibano hicho
kinamuhusu mtu yeyote mwenye shughuli mahakamani hapo wakiwemo mashahidi,
wasikilizaji wa kesi na wanahohitaji huduma mbalimbali.
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kweyi Rusemwa aliliambia gazeti hili jana Dar es
Salaam kuwa mavazi hayo yanashusha heshima na hivyo watahakikisha wanaofika
mahakamani hapo wanabadilika kimtazamo.
“Kama
mtu anakuja kwa ajili ya Mahakama lazima avae mavazi ambayo si kero kwa
mwingine. Wanaofika hapa wakiwa na mavazi yasiyostahili wataishia nje,’’
alisema Rusemwa.
Alitahadharisha
anayefika mahakamani kuwa na khanga ili akibainika vazi alilovaa halistahili,
aweze kujisitiri kwa kufunga khanga hiyo na kuingia mahakamani kupata
huduma.
Alisema
tatizo la mavazi yasiyostahili limekuwa kubwa hususani miongoni mwa wanawake
ambao baadhi hawatambui thamani yao kwa kuamua kuvaa mavazi yasiyo na heshima.
Hata
hivyo, alisema kwa upande wa washitakiwa, ipo changamoto kubwa kwao katika
kudhibiti uvaaji usiofaa.
Alitoa
mfano wa watu wanaofikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuuza miili yao, kwamba
wengi hukamatwa wakiwa nusu uchi na kwamba inapotokea wakafikishwa mahakamani,
hushindwa kuwarudisha.
Mwandishi
wa habari hii alishuhudia baadhi ya wanawake waliorudishwa langoni ambao baadhi
walikuwa wakihaha kuomba khanga ili waruhusiwe kuingia mahakamani.
Pamoja
na walinzi kudhibiti mavazi hayo mlangoni, vile vile matangazo yamewekwa
kuelekeza wageni wanaofika hapo kuzingatia masharti hayo ya uvaaji.
No comments:
Post a Comment