WACHIMBAJI WADOGO WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA NISHATI


Wachimbaji wadogo wa madini wamepongeza Utendaji Kazi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa kuondoa migogoro iliyokuwepo ya kupata maeneo ya uchimbaji pamoja na kupatiwa ruzuku. 
Huku wakiwasihi wachimbaji hao nchini kuachana na siasa na kupanga mikakati ya kuwezesha ukombozi ulioanza, wameeleza kuwa baada ya wizara hiyo kuongozwa na Profesa Sospeter Muhongo yamebadilisha maisha ya wachimbaji hao kujitambua kibiashara huku wakiwa na umoja wa kuaminika unaowawezesha kupata ruzuku na baadaye kupewa mikopo na Benki ya TIB. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa wachimbaji wadogo wanawake, Sarah Msambagula alisema baada ya waziri huyo kuanza kazi amesaidia wachimbaji hao kuwa na uongozi kwa kila mkoa. 
Huku Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Manyoni, Francis Mbassa akisifu juhudi hizo za wizara kwa kuwapatia leseni tatu za uchimbaji, wachimbaji wadogo wa kikundi cha ushirika cha Aminika Gold Mine na kupewa ruzuku ya dola za Marekani 25,000. 
Alisema kwa sasa anaomba serikali kuendelea kuwasaidia kupata mikopo zaidi ili kufanya uchimbaji unaofaa wa kisasa na siyo sasa wanapotumia vifaa duni.

No comments: