MAREKANI KUENDELEA KUSAIDIA MAENDELEO


Serikali ya Marekani imehakikishia Tanzania kwamba itadumisha uhusiano kudumisha  na kazi iliyoko mbele ni kuhakikisha inapiga hatua zaidi na siyo kurudi nyuma. 
Balozi Mark Childress alisema hayo jana alipokutaka na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal  alipokwenda kujitambulisha. 
Childress ambaye ni balozi wa Marekani nchini,  alisema Tanzania ni nchi yenye uhusiano na Marekani na kwamba katika kipindi chake atahakikisha uhusiano huo mzuri uliojengwa unadumishwa. 
“Nchi hizi mbili zina uhusiano maridhawa, katika kipindi changu atahakikisha uhusiano huu unadumishwa na nchi hizi mbili zinazidi kuwa na maeneo ya kushirikiana hasa yanayolenga kuboresha maisha ya watu na kuwapatia maendeleo.” 
Alisema Tanzania imekuwa ikitumika kama mfano kutokana na  kuonesha mabadiliko ya haraka katika miradi mbalimbali inayoendeshwa kwa ushirikiano na watu wa Marekani na akafafanua kuwa, kazi iliyoko mbele ni kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua zaidi na sio kurudi nyuma. 
“ Kila nikipata fursa ya kukutana na wenzangu tumekuwa tukizungumzia suala la Tanzania kupiga hatua kwa haraka. Mna mambo mengi yaliyofanyika na kazi iliyopo ni kuendelea kupiga hatua pasipo kurudi nyuma,” alisema. 
Makamu wa Rais, Bilal alimweleza Balozi Childress kuwa, Tanzania ipo katika kipindi ambacho kinaonesha mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kwamba kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa na unasaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

No comments: