Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge leo atafungua
maadhimisho ya siku ya Mazingira dunia yatakayofanyika kitaifa katika mkoani
hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Baraka
Konisaga alisema maadhimisho hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Furahisha,
jijini hapa ambapo hadi kilele chake Juni 5, mwaka huu wageni kutoka ndani na
nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki.
Alisema
katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya 'Tunza mazingira ili kukabiliana na
tabia nchi' inahimiza juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi kuwa na changamoto mbalimbali katika taifa.
Alisema
katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na
kufanya usafi, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira kwa njia ya
makongamano, kupanda miti, kuzoa takataka, kuondoa magugu maji katika ziwa
Victoria na ufugaji wa nyuki.
Naye
Naibu Katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Anjelina Madete alisema
mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na ges joto ambazo hutokana na shughuli
za maendeleo kama vile viwanda ambazo zimeongezeka kwenye uso wa dunia.
Alisema
mabadiliko hayo yameleta athari mbalimbali zikiwemo za kutotabilika kwa majira
ya mvua,kutishia visiwa kutoweka, maeneo ya misitu mikubwa kupungua kutoka na
na bionuai.
No comments:
Post a Comment