DIT KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI 2,000

Zaidi ya wajasiriamali wadogo 2,000 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatarajiwa kupewa mafunzo maalumu ya ujasiriamali kwa ajili ya
kukuza biashara zao na kuhimiri ushindani ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Msimamizi wa mafunzo hayo na Mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam(DIT) Amos Nungu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa wakufunzi wa wajasirimali hao.
“Hii ni awamu ya pili ya mafunzo haya, awali tulitoa mafunzo  mengine kama haya yaliyokuwa yamewalenga watu wa kawaida ili waweze kuwa wajasiriamali kupitia mpango uliotambulika kama ‘Kazi Nje Nje’ ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kuleta mabadiliko” alisema Nungu.
Aidha aliitaja mikoa ambayo elimu hiyo inatarajiwa kutolewa kuwa ni pamoja na Pwani Arusha,Morogoro, Iringa,Mwanza,Mbeya pamoja na Mtwara na kusisitiza kuwa kupitia utaratibu huo, imani yao wajasiriamali hao wataweza kukuza mitaji yao na kuongeza ushindani katika biashara wanazozifanya.

No comments: