Wasomi, wanaharakati na wananchi kwa
ujumla wamepongeza Bajeti ya mwaka 2014/15 ya Sh trilioni 19 iliyowasilishwa
bungeni juzi na kujikita zaidi katika kuimarisha miundombinu ya elimu, usafiri
wa reli na usambazaji wa nishati ya umeme vijijini, wakisema imekata kiu ya
Watanzania wengi.
Aidha, wamepongeza hatua ya kuondoa
misamaha ya kodi katika maeneo muhimu na kusema hali hiyo inaonesha kuimarika
kwa wizara hiyo katika suala la kuhakikisha taifa linakua kiuchumi.
Akizungumza na gazeti hilo jijini
Dar es Salaam jana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Benson Bana
alisema maandalizi ya bajeti ya mwaka huu yanaonesha yaliandaliwa vizuri na
kwamba wameangalia jinsi ya kugharimia bajeti ya maendeleo kwa kutumia vyanzo
vya ndani.
Dk Bana alisema, kikubwa kinachofurahisha
katika bajeti hiyo ni kwamba Wizara imeangalia mambo muhimu na kuyatengea
bajeti ambapo kwa upande wa bajeti ya maendeleo, Serikali imeainisha vyanzo vya
ndani katika kupata fedha za bajeti hiyo, badala ya kutegemea fedha kutoka kwa
wahisani.
“Ni jambo zuri na tunapaswa
kuwapongeza Serikali kwa kuona hili, inaonesha Wizara imeimarika na
walijiandaa,” alisema Dk Bana.
Akizungumzia kuhusu kupunguza
misamaha ya kodi, Dk Bana alisema ni jambo jema kwa wizara kuona haja ya
kufanya hivyo kwani, baadhi ya misamaha iliyokuwa ikitolewa haikuleta tija kwa
maendeleo ya taifa.
Alisema hatua hiyo hivi sasa
itajenga uwajibikaji na uwazi kwa watendaji wa Serikali kwani kwa
watakaosamehewa kodi watatangazwa na kujulikana kama misamaha yao ina tija au
la.
Kuhusu, mishahara na vipaumbele vya
Serikali, Dk Bana alisema kuweka vipaumbele ni jambo jema ambapo kwa kuangalia
hili Serikali imetenga jumla ya Sh trilioni 3.4 kwenye sekta ya elimu
ambayo ndiyo imetengewa fedha nyingi kuliko zote.
Alisema jambo hilo litaisadia
kuboresha sekta hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na kuonya kuwa
ni vyema wanaopata mikopo ya masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,
mara wamalizapo warudishe mkopo waliopewa.
“Tujenge tabia ya kulipa, ili na
wengine wakopeshwe. Umepewa mkopo umesoma umemaliza una kazi au huna kazi,
lakini angalia jinsi ya kurejesha mkopo ili wengine nao wasome,” alisisitiza Dk
Bana.
Pamoja na kusifu bajeti hiyo, Dk
Bana aliikosoa kwa kusema haikuonesha vyanzo vipya vya mapato na kusisitiza
kwamba Serikali ingekuwa na mtazamo wa kuangalia sekta na watu binafsi kuona
mchango wao katika pato la Taifa ni upi na kama wanalipa kodi inavyostahili.
Alisema ni vyema hata posho za
wabunge zingepaswa kukatwa kodi ili kupata chanzo kipya cha kodi na pia hata ruzuku
za vyama vya siasa nazo zingekuwa zinakatwa kodi.
Alisema kufanya hivyo kuwaongeza
vyanzo vya fedha na kupunguza mzigo mzito kwa wananchi hasa wa kodi na
ushuru kwenye bidhaa za lazima kama vile, saruji, mabati na mafuta ambazo
zinapoongezeka kodi zinaathiri maisha ya wananchi wengi hususan wa vijijini.
Naye Mtaalamu wa Uchumi ambaye ni
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Haji Semboja alisema kupungua kwa
makato ya kodi ni jambo zuri na la heri kwa kuwa itaongeza vipato kwa wananchi
wenye ajira. Pia alisema uamuzi wa serikali na taasisi zake kuagiza vifaa kwa
pamoja ni jambo jema kwani litapunguza mianya ya rushwa na ubadhirifu wa fedha
za umma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk Hellen Kijjo Bisimba alisema
pamoja na mipango mizuri ya Serikali kwenye bajeti hiyo, lakini haikuja na
vyanzo mbadala vya mapato.
Alisema kuendelea kuongeza kodi
kwenye vileo kama vile pombe na sigara, vinaweza kuathiri familia nyingi ambapo
wazazi au walezi wa familia hizo nao watapunguza kiwango cha fedha za matumizi
ya nyumbani ili kubaki na fedha za vileo.
“Kama awali baba au mama alikuwa
anaacha Sh 10,000 ya matumizi kwa siku nyumbani hivi sasa itabidi aache 8,000
ili abakiwe na fedha kwa ajili ya kileo na sigara ambavyo vimeongezwa kodi,
sasa hii ni kutesa familia,” alisema Dk Bisimba.
Dk Bisimba aliongeza, katika
hilo familia ndizo zitapata shida kwa kuwa si rahisi ulevi kwisha
na badala yake wataendelea kunywa, lakini kama serikali ingebuni vyanzo
vingine vya mapato na kuacha kuongeza kodi kwenye vileo ingekuwa bora zaidi.
Hata hivyo, alisema bajeti ya afya
pamoja na kutengewa fedha Sh trilioni 1.5 bado kiwango hicho ni kidogo kwa
kulinganisha na makubaliano ya nchi za Afrika Mashariki kuwa asilimia 15 ya
bajeti itengwe kwa ajili ya sekta ya afya.
Bajeti kuu ya Serikali ilitangazwa
juzi bungeni ya Sh trilioni 19.87 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa
Fedha, Saada Salum Mkuya huku ikiwabana wananchi katika bidhaa na huduma
za starehe huku ikitoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu.
Kwa upande wa Waziri Mkuu mstaafu,
Dk John Malecela alisema bajeti ya mwaka huu imekuwa na mambo mengi muhimu
yaliyokuwa yakihitajika kwa wananchi.
Pongezi nyingine zimetoka kwa Mbunge
wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
aliyesema bajeti imezingatia mambo muhimu ikiwa pamoja na kupunguza misamaha ya
kodi, jambo alilosema ni la maana. Lakini alinung’unikia punguzo dogo la kodi
wanayotozwa wafanyakazi katika mishahara, punguzo la asilimia moja kutoka 13
hadi 12 bado ni ndogo, hivyo linapaswa kupungua zaidi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Vyama Huru vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicholas Mgaya alisema pamoja na punguzo la
kodi katika mishahara, bado serikali inapaswa kuendelea kushusha na kufikia
digiti moja, yaani chini ya asilimia 10.
Aidha, alisema ahadi ya kuongeza
kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma itakuwa hatua nzuri kutokana
na kile alichosema kiwango cha mshahara wanaolipwa hauendani na hali halisi ya
maisha ya Mtanzania kwa sasa.
Kwa ujumla, wananchi wengi
waliozungumza na gazeti hili walielezea kufurahishwa na bajeti, hasa kwa uamuzi
wa kufyeka misamaha ya kodi wakisema itasaidia kuongeza kukuza uchumi wa nchi,
hivyo kuchochea kasi ya maendeleo na pia kupunguza makali ya maisha.
1 comment:
Natalie Cuttaia
Siwezi kuficha ushahidi huu mkubwa yanayotokea katika maisha yangu mimi upendo kila mtu kujua na kuwa na mshirika kwamba ni kwa nini mimi daima mahali ni juu ya jibu, mimi Bibi, Natalie Cuttaia kwa jina, mimi kuishi katika Texas, Umoja wa Nchi Of America, nataka kuwashukuru (Mr Richard Raymond) kwa wema wake juu ya maisha ya familia yangu.
Sikujua kwamba bado kuna ni nzuri Taasisi kama hii kwenye mtandao na duniani hapa. Baadhi tu Miezi Back, nilikuwa katika kutafuta mkopo wa $ 100,000,00 kama mimi nilikuwa mbio nje ya fedha kwa ajili ya chakula na kodi. Mimi nilikuwa scammed $ 6,800 Dola na niliamua si kuhusisha yangu binafsi katika biashara hiyo tena lakini Friend yangu ilianzisha mimi kwa kampuni mkopo kutokana na muonekano wangu na matendo.
Na mimi kumwambia kuwa mimi si nia ya mpango wowote mkopo tena lakini yeye aliniambia kuwa bado kuna Taasisi nzuri nani atakuwa kupendekeza mimi, na mimi alifanya kesi na mimi zaidi kushukuru bahati mimi leo, nilipewa kiasi cha mkopo wa $ 100,000.00usd, na Kampuni hii kubwa (Bruce Brandon Loan Company) kusimamiwa na (Mr.Bruce Brandon) Kama wewe ni katika haja ya kweli au legit mkopo au msaada wa kifedha na unaweza kuwa kuaminika na kuaminiwa ya uwezo wa kulipa nyuma kwa wakati kutokana wa fedha nami ushauri wewe, kuwasiliana naye kupitia: (bruce.brandon071@gmail.com) Na utakuwa huru kutoka scams katika internet.
All shukrani kwa Mr.Bruce Brandon Wewe ni mmoja ambaye kuondoa mimi na familia yangu kutoka katika umaskini. Sababu i am kufanya hii ni kwamba, i ahadi Mr.Bruce Brandon kwamba kama i kweli got mkopo wangu, i itakuwa advertize kampuni yake na kuleta wateja kwa kampuni yake. Kuwasiliana naye kupitia (citiloanfinancelimited@gmail.com) kwa ajili ya mikopo ya umekuwa kutafuta kwa ..
Post a Comment