ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUNAJISI MBUZI UKEREWE



Mtu mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi.
Mtuhumiwa huyo, William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo,  Faustine  Kishenyi.
Mwendesha  Mashitaka wa  Polisi,  Inspekta  Samwel  Onyango  aliieleza mahakama hiyo kuwa  mshitakiwa huyo  alitenda kosa  hilo  Juni 4 mwaka huu saa 9 alasiri  huko Mlezi, Ukerewe.
Katika hati ya mashitaka  imeelezwa  kuwa  mshitakiwa huyo  alikutwa  akitenda kosa hilo katika banda la mbuzi nyumbani kwao  na  mmoja  wa wanafamilia.
Katika maelezo hayo,  Onyango  alisema mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la  tatu katika Shule ya Msingi  Mlezi, baada ya kushuhudia tukio hilo alikwenda kutoa taarifa kwa baba yao,  Maxmilian Stephan  aliyefika na kumkuta mtuhumiwa akiendelea `kuhangaika' na mbuzi huyo.
Akifafanua,  alisema  kosa hilo ni kinyume cha sheria  ya makosa la  kujamiiana  kifungu namba  K/F 154 (1) na (2) C  sura   ya 16  ya marekebisho ya sheria  ya mwaka 2002.
Mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.

No comments: