WATUHUMIWA WA MABOMU ARUSHA HAWAHUSIANI NA MAKUNDI YA KIGAIDI


Jeshi la polisi limesema watuhumiwa waliokamatwa  katika tukio la mabomu lilitokea Arusha Aprili 13  hawahusiani na kundi lolote la kigaidi.  
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai, Isaya Mungulu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema kuna baadhi ya vyombo vya habari vimewahusisha watuhumiwa hao na makundi ya kigaidi kama Al-shabaab. 
Aidha katika taarifa yake aliyoitoa jana jijini Arusha, alisema hakuna mahali ambapo alitaja watuhumiwa hao wana uhusiano na kundi la kigaidi. 
“Kuna ambao walitoa habari kwa maelezo niliyotoa ila wengine waliamua kutoa tofauti na maongezi yangu,” alisema Mungulu. 
Pia alitoa mwito kwa vyombo vyote vya habari, wakiwemo waandishi wa habari kuwa makini na taarifa wanazozitoa ama kuripoti hususani kuzingatia weledi wa taaluma yao unaowataka kuripoti kile kilichotolewa na mtoa taarifa pasipo kuongeza neno lolote.

No comments: