NYARAKA, KOMPYUTA ZA GAZETI ZAIBWA

Ofisi za Gazeti la Daraja Letu, zilizopo eneo la Uwanja wa Ndege mjini Njombe, zimevunjwa na kuibwa nyaraka muhimu mbalimbali na kompyuta tano.
Akizungumzia wizi huo kwa mwandishi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Daraja, ambalo ni wachapishaji wa gazeti hilo, Simon Mkina alisema wizi huo uliotokea usiku wa Aprili 30, mwaka huu.
Alisema kufuatia wizi huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu wawili kwa uchunguzi zaidi.
Akizungumzia mazingira ya wizi huo, Mkina alisema dalili zinaonesha kuwaulipangwa ama na baadhi ya watu wanaojua vyema taratibu za kazi za shirikalake, au watu wenye uhusiano wa karibu na ofisi hiyo.
"Kuna uwezekano mkubwa wa kuhusika kwa watu wa karibu na shirika letu, lakini kwa kuwa tayari Polisi imeanza kazi zake, ni vyema tukaliacha Jeshihilo likaendelea na matokeo yake tutaambiwa," aliongeza Mkina.
Mkurugenzi huyo pia alisema huenda asili ya kazi za gazeti lao, hasa habariza uchunguzi, ikawa sababu nyingine ya wahusika wa wizi huo wa nyarakakuhusika.
"Siwezi kueleza moja kwa moja iwapo habari zetu za uchunguzi zikawa chanzopia, lakini si chanzo cha kupuuza, maana utendaji wetu umekuwa mwiba kwawatendaji wabovu wa Halmashauri," alisema Mkina.
Gazeti la Daraja Letu limekuwa likiandika habari za utendaji usioridhishawa baadhi ya viongozi wa halmashauri za mikoa ya Njombe na Iringa, kufuatilia matumizi ya fedha na pia kuibua changamoto za maisha namaendeleo kwa mikoa hiyo miwili.

No comments: