MKURUGENZI STAR CITY HOTEL ATAKA WAWEKEZAJI WAZAWA WAPEWE KIPAUMBELE

Mkurugenzi wa Hoteli ya Star City, Obadia Mtewele ameiomba serikali kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuleta maendeleo ya nchi.
Mtewele alisema hayo hivi karibuni Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa hoteli yake hiyo iliyopo Sinza.
Alisema ni vyema serikali ikawaunga mkono wawekezaji wazawa kuliko wa nje ili vijana wengi wenye malengo watumie fursa hiyo kujiari wenyewe na kuleta maendeleo ya nchi.“
Unapomwezesha mzawa, nchi inakuwa na wawekezaji wengi kutoka ndani pia tunaleta maendeleo ya nchi kwa kuwa tunatoa ajira kwa vijana na kulipa kodi,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Ofisa Utumishi Mkuu wa Wilaya hiyo, Godfrey Mgomi alisema sera na sheria hazimzuii mtu kuwekeza bali kuna utaratibu anatakiwa aufuate.
Aliwataka vijana kutumia fursa zilizopo kufanya uwekezaji kama alivyofanya Mtewele ambaye amejenga hoteli na kutoa ajira kwa watu 21 pamoja na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi.

No comments: