Mandhari ya Saluni ya BM kwa nje. |
Saluni ya BM Hair and Beauty Clinic leo imeadhimisha miaka 11 tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2002 Kinondoni Manyanya, Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi Mkurugenzi wa saluni hiyo, Benno Chelele alisema kuwa saluni hiyo ni ya kimataifa na ni moja ya saluni kubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
“Sijui kwa sehemu nyingine za Afrika kama Afrika Kusini, Nigeria na kwingineko lakini nina uhakika kwa Afrika Mashariki saluni yetu inaongoza,” alisema Chelele.
Alisema moja ya malengo yao ni kujitanua sehemu nyingine za Tanzania na kufanya uwekezaji kupitia biashara hiyo katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi katika miaka kumi inayokuja.
Chelele akielezea mafanikio ya saluni yake alisema ni pamoja na kuwapeleka Afrika Kusini wafanyakazi wake kuhudhuria mafunzo na kuwafanya waweze kuhudumia wateja katika viwango vya kimataifa.
“Mara kwa mara tunawapeleka wafanyakazi wetu Afrika Kusini kusomea mambo haya, kwani mitindo na staili zake hubadilika kila mara na kuwafanya wawe na viwango vya kimataifa kwani tulishatoka muda mrefu katika kuhudumia kwa viwango vya kawaida,” alisema Chelele.
Katika hatua nyingine, saluni hiyo ilitoa tuzo ya wafanyakazi bora ambazo zilitolewa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benno Chelele.
Waliopewa tuzo hizo ni Hassan Hassani ambaye alipewa tuzo ya mfanyakazi bora wa jumla ambapo alipewa zawadi ya saa yenye thamani ya Sh 500,000, wengine ni Regina Sebastian aliyepata microwave yenye thamani ya Sh 250,000, Diana Kyaruzi alipata saa yenye thamani ya Sh 150,000 na Benard Samwel na Ramadhani Fundi waliopata fedha taslimu Sh 50,000 kila mmoja.

No comments:
Post a Comment