WILSHERE ASEMA SIGARA ALIYOBAMBWA AKIVUTA NDIYO YA MWISHO...

Kiungo wa timu ya soka ya Arsenal ya England, Jack Wilshere, amekiri hadharani kwamba kukutwa kwake wiki iliyopita akivuta sigara nje ya klabu moja ya usiku lilikuwa 'kosa'.
Mchezaji huyo ameenda mbali zaidi katika kile kinachoonekana kujutia kitendo hicho kwa kusema ile inaweza kuwa ndio sigara yake ya mwisho.
Wilshere, ambaye ambaye amerejea hivi karibuni kikosini kwa Washika Bunduki hao wa London baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu, ameshutumiwa vikali baada ya picha yake akivuta sigara kuchapishwa kwenye gazeti moja na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Meneja wa Arsenal. Arsene Wenger amenukuliwa kusema amechukizwa mno na kitendo cha kiungo wake huyo na kwamba atamkalisha chini kumfunda.
Mbali na hilo, Wenger ameshaweka bayana kwamba pamoja na tukio hilo, bado Wilshere ataendelea kuwa katika kikosi cha kwanza cha timu yake.

No comments: