Tundu Lissu. |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema iwapo Rais Jakaya Kikwete ana nia ya kumaliza mvutano unaoendelea juu ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 kwa mazungumzo hana budi kutousaini muswada huo.
Chama hicho kimesisitiza kuwa iwapo Rais atausaini muswada huo vyama vya upinzani nchini havitokuwa tayari kukaa mezani kumaliza suala hilo, na kwamba hali hiyo ikiendelea nchi itaingia kwenye machafuko.
Hayo yalisemwa jana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Alisema katika hotuba hiyo Rais Kikwete alibainisha kuwa ana nia ya kumaliza mvutano unaoendelea kuhusu muswada huo uliopitishwa katika mkutano uliopita wa Bunge na wabunge wa chama tawala pekee baada ya wabunge wote wa upinzani kususia mjadala wa kupitishwa kwake.
“Sasa mimi nasisitiza kuwa kama kweli Rais yuko makini na ana nia ya kumaliza mvutano huu na kuwezesha mchakato wa mabadiliko ya katiba kuendelea kama kawaida, basi asisaini kwanza muswada huu ndio azungumze na sisi, akiusaini tu hakutakuwa na mazungumzo yoyote,” alisisitiza.
Alisema haitokuwa na maana yoyote kuendelea na mazungumzo baada ya Rais kusaini na kuidhinisha muswada huo ambao kwa sasa unapigiwa kelele kuwa una mapungufu makubwa ambayo yakiachwa kuna hatari ya kupatikana Katiba mbovu au kuibuka kwa machafuko kama yaliyotokea katika nchi za Kenya na Zimbabwe.
“Rais ana mamlaka ya kukataa kupitisha mambo ya kijinga na huu muswada nawaambia umejaa ujinga, Tanzania imeingia makubaliano na Marekani ya kutoidhinisha mambo yasiyo na tija, tunamuomba Kikwete atumie fursa hiyo kwa kuidhinisha muswada huu kwa kuwa hauna tija kwa taifa hili,” alisisitiza.
Akijibu hotuba ya Rais Kikwete dhidi yake aliyoitoa mwishoni mwa mwezi huu, kuwa mbunge huyo ni muongo na mzandiki kudai kuwa Rais hakuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Lissu alisisitiza kuwa aliyayosema ni kweli na hajali kuitwa muongo.

No comments:
Post a Comment