MJANE GAIDI WA UINGEREZA AHOFIWA KUFA UTEKAJI WESTGATE SHOPPING MALL...

Samantha Lewthwaite.
'Mjane Mweupe' Samantha Lewthwaite anawezekana kuwa ameuawa katika utekaji nyara wa Nairobi.

Huku jaribio la kuwateketeza wanamgambo waliobaki kwenye Kituo cha Biashara cha Kenya likiendelea, maofisa walisema Waislamu watatu wenye msimamo mkali wamekufa katika majaribio ya kuwaachia mateka wao.
Watu wa ndani walisema mmoja alikuwa mwanamke mweupe - wakiongezea uzito katika maelezo yao kwamba ni Lewthwaite, mjane wa mlipuaji mabomu ya 7/7 Jermaine Lindsay, alishiriki kwenye shambulio hilo ambalo limesababisha vifo vya watu 62 na wengine 170 kujeruhiwa.
Sehemu ya kundi hilo iliyofanya shambulio hilo katika jengo hilo iliundwa na raia wa Marekani, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed.
Maofisa wa Marekani walisema wanatazama kama kuna Mmarekani yeyote alihusika. Msemaji wa Ikulu Jen Psaki alisema Jumatatu idara hiyo haina 'ushahidi wa moja kwa moja wa utaifa au utambulisho' wa washambulizi hao.
Ikulu ya Uingereza ilisema takribani watu sita waliokufa ni Waingereza na kuonya kwamba kulikuwa na 'uwezekano zaidi wa taarifa mbaya'.
Ripoti kutoka Reuters zilisema vyanzo vitatu - moja ofisa wa usalama wa taifa na wanajeshi wawili - umethibitisha kwamba mwanamke mmoja mweupe alikuwa miongoni mwa magaidi waliouawa.
Polisi wanaperuzi kama alikuwa mateka aliyevalia nguo za mmoja wa magaidi hao, lakini Wizara ya Mambo ya Nje pia inachunguza mitandao ya Lewthwaite ambaye alibadili dini na kuwa Muislamu katika mauaji hayo.
Mama huyo wa watoto wanne mwenye miaka 29, kutoka Home Counties, sasa ni mtu maarufu katika Al-Shabaab - kundi la kigaidi lililodai kuhusika na mauaji hayo katika kituo cha biashara cha Westgate kinachomilikiwa na raia wa Israeli.
Polisi wanaamini ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa kundi hilo na mwalimu wa kutengeneza mabomu. Hatahivyo, vyanzo vinakiri bado hawafahamu ushiriki wake kamili kwenye shambulio la Nairobi.
Isitoshe, ofisa mmoja wa kupambana na ugaidi Kenya jana alidai: "Tunaamini alikuwa kiongozi wa operesheni hiyo lakini nafasi yake bado haijafahamika. Inafahamika alikuwa pia mdunguaji."
Ilibainika juzi kwamba askari wamesema waliona mwanamke mweupe akiwa amejifunga ushungi akitoa amri kwa watu wenye silaha kwa lugha ya Kiarabu.
Licha ya hili, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku alisema kwamba magaidi wote hao walikuwa wanaume, huku baadhi yao wakiwa wamevalia kama wanawake. Lewthwaite amekuwa akiruka huku na huko katika Afrika Mashariki tangu polisi kufichua mpango wake wa kulipua kituo cha biashara katika mji mwingine wa Kenya, Mombasa, miaka miwili iliyopita.
Mwenzake mzaliwa wa London, Jermaine Grant, alitarajiwa kupanda kizimbani juzi, lakini kesi yake ilisitishwa kwa muda ili kuwezesha maofisa kwenda Nairobi, kusaidia maofisa huko.

No comments: