VIFAA VYAANGUKA KUTOKA KWENYE INJINI YA NDEGE YENYE ABIRIA 256 IKIWA ANGANI...

Ndege hiyo baada ya kutua kwenye Uwanja wa Hearthrow.
Vifaa vya injini ya ndege vimeanguka kutoka umbali wa futi 15,000 kwenye kijiji cha Heretfordshire wakati ikishika kasi kutoka Uwanja wa ndege wa Heathrow, kwa mujibu wa uchunguzi.

Mabaki hayo mvunjiko yalitoka kwenye ndege aina ya Boeing 777 iliyokuwa ikielekea Dubai ambayo ilikuwa na abiria 256 na wafanyakazi 12 ndani yake.
Muda mchache baada ya kuruka Desemba mwaka jana, wafanyakazi walisikia 'kwa sauti kubwa, kelele za mrindimo' na mtikisiko ukitokea kwenye moja kati ya injini mbili za Rolls Royce Trent.
Rubani huyo mwenye miaka 56 wa ndege ya Royal Brunei Airlines aliamua kugeuza na kurudi uwanja wa ndege kama tahadhari, ambako wahandisi waligundua sehemu ya injini haikuwapo.
Baadaye iligundulika kwamba vifaa hivyo vilianguka kwenye kijiji cha Broxbourne, huko Hertfordshire.
Sehemu kuu ya injini iliyovunjika iliangukia kwenye jengo moja katika kijiji hicho, ripoti kutoka Tawi la Idara ya Usafiri la Uchunguzi wa Ajali za Ndege ilisema.
Sasa watengenezaji wa injini hiyo wameanzisha uchunguzi kuhusu jinsi injini hiyo ya upande wa kulia ilivyoharibika.
Ripoti hiyo ilisema: "Hili ni tukio la kumi na tano la kufanana linalojulikana na mtengenezaji.
"Mtengenezaji wa ndege hiyo ameshauri kwamba ukuta wa ndani wa injini hiyo utahitajika kubadilishwa na pengine amri kwa ndege zote zilizoathirika.
"Idadi ya vifaa vilivyopotea kwenye injini hiyo vilipatikana baadaye siku hiyo kutoka kwenye nyumba moja mjini Broxbourne."
Hakuna abiria au mfanyakazi aliyedhurika katika tukio hilo na inaaminika kwamba hakuna yeyote kwenye kijiji hicho aliyejeruhiwa.

No comments: