KUSHOTO: Majeraha ya mmoja wa mabinti hao. KULIA: Ndege iliyowabeba mabinti hao ikitua kwenye Uwanja wa RAF Northolt jana ikitokea mjini Dar es Salaam. |
Baba aliyeumizwa mno wa mmoja wa wasichana wa Uingereza wajeruhiwa vibaya katika shambulio la tindikali mjini Zanzibar amefichua majeraha ya binti yake huyo kwamba 'ya kutisha mno' na 'kuliko inavyodhaniwa'.
Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye miaka 18, waliwasili nchini Uingereza jana mchana pale ndege ilipotua kwenye Uwanja wa RAF Northolt. Haraka wakasafirishwa kwenda hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa, huku wakisindikizwa na jamaa zao.
Baba wa Katie, Jeremy Gee, alielezea machungu ya familia hiyo baada ya picha ya kwanza ya majeraha hayo ya moto yaliyompata mmoja wa wasichana hao kuwekwa hadharani.
Alisema: "Picha hizo nilizoziona hakika ni za kutisha mno.
"Kiwango cha kuungua ni zaidi ya unavyoweza kudhani."
Wasichana hao wote wa Uingereza wamepata majeraha makubwa ya moto pale tindikali ilivyomwagwa kwenye nyuso zao wakati wakitembea kwenda kwenye mgahawa mmoja katika kisiwa chenye waumini wengi wa Kiislamu cha Zanzibar.
Lilikuwa shambulio la tatu kwao katika kipindi walichokaa kwenye kisiwa hicho.
Polisi wamebainisha kwamba watuhumiwa watano walikamatwa juzi Alhamisi na mapema jana asubuhi kwenye eneo la Mji Mkongwe, ambako Kirstie Trup na Katie Gee walishambuliwa, ofisa wa ngazi ya juu alieleza.
Na donge nono la Pauni za Uingereza 4,000 limetangazwa na polisi Zanzibar kwa yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa shambulio hilo, kwa mujibu wa BBC.
Polisi pia imetoa hati ya kukamatwa kwa Mhubiri wa Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, kwa hisia kwamba mafundisho yake yanaweza kuwa yanachochea mashambulio ya tindikali.
Marafiki wa wasichana hao wamehisi huenda walishambuliwa kwakuwa ni Wayahudi, na polisi wa kisiwani humo walisema wanataka kuzungumza na mhubiri huyo wa Kiislamu ambaye anawezekana kuwa alichochea shambulio hilo.
Wakiwasili ndani ya gari aina ya Audi jeusi kwenye uwanja wa ndege wa jeshi jana asubuhi mama wa Katie aliyeguswa mno, Nicky aliweka bayana mateso ya familia hiyo.
Akizungumza wakati wakikaribia kuingiwa uwanjani hapo alisema: "Nimejawa na hofu. Imekuwa mateso makubwa kwa familia zetu. Ninafurahi kwamba amerejea nyumbani. Ninataka kuingia ndani na kumwona.
"Tulizungumza asubuhi hii na alisema yuko salama. Sifahamu kabisa kinachoendelea.
"Siwezi kusema zaidi sababu tunatakiwa kuingia ndani na kuwaona wote."
Wafanyakazi wawili kutoka magari ya wagonjwa ya St John waliwasili kwenye makao makuu ya jeshi ya Middlesex, ambako pia hupokea ndege binafsi, majira ya Saa 4 asubuhi jana.
No comments:
Post a Comment