ALIYEKUWA AUAWE KESHOKUTWA AKUTWA KAJINYONGA JELA...

Billy Slagle.
Muuaji anayekabiliwa na adhabu ya kifo Jumatano ya wiki hii, amekutwa amenyongwa kwenye selo yake Jumapili, Ohio alikokuwa akisubiria kutekelezwa kwa hukumu yake ya kifo, maofisa wa gereza wamesema.

Msemaji wa magereza JoEllen Smith alisema Billy Slagle, mwenye umri wa miaka 44, alikutwa akining'inia kwenye selo yake majira ya Saa 11 alfajiri katika Taasisi ya Kurekebisha Tabia ya Chillicothe kusini mwa Columbus.
Alitangazwa kufariki ndani ya saa moja.
Hakuna taarifa nyingine zaidi zilizopatikana haraka.
Slagle alikuwa amehukumiwa kifo kwa kumchoma visu jirani yake Mari Anne Pope mwaka 1987 katika ujambazi uliotokea huko Cleveland huku watoto wadogo wawili wakiwa wanashuhudia.
Katika uamuzi nadra kutokea, Mwendesha mashitaka huko Cleveland aliitaka Bodi ya Parole ya Ohio kumweka kiporo Slagle.

No comments: