Chris Kelly, mmoja wa wasanii wawili wa kundi la Kriss Kross lililotamba katika miaka ya 1990 ambao walidumu kwa miaka 10 ya nyimbo za kukumbukwa kikiwamo kibao cha "Jump", amefariki dunia mapema leo kwenye hospitali moja mjini Atlanta kwa kile kinachodaiwa kujizidishia dozi ya dawa nyumbani kwake, imeelezwa. Alikuwa na umri wa miaka 34.
"Inaonesha kuna uwezekano wa kuzidisha dozi ya dawa," alisema Koplo Kay Lester, msemaji wa Polisi wa Fulton County.
Hii, alisema Lester, inatokana na taarifa zilizopokelewa kwenye eneo la tukio na pia ushahidi uliopatikana nyumbani kwa Kelly huko kusini Atlanta.
Kwa mujibu wa Lester, polisi waliitwa nyumbani kwa Kelly majira ya mchana. Alipelekwa kwenda Kituo cha Afya cha Atlanta.
Mchunguzi Betty Heney wa Ofisi ya uchunguzi ya Fulton County alisema Kelly alitangazwa kufa katika hospitali hiyo mapema leo.
Hakuna sababu rasmi za kifo chake zilizoelezwa, kusubiria uchunguzi.
Kelly, aliyefahamika kama "Mac Daddy," na Chris Smith, alifahamika kama "Daddy Mac," walivumbuliwa kwenye ulimwengu wa muziki mwaka 1992 na prodyuza wa muziki na rapa Jermaine Dupri baada ya kuwagundua wawili hao kwenye ukumbi mmoja mjini Atlanta. Wawili hao walikuwa wakivaa nguo zao kinyume, lakini waliweza kuwateka mashabiki kwa rapu zao.
Wimbo wao wa kwanza uliowapatia mafanikio makubwa ulikuwa "Jump." Kibao hicho kilikuwa kwenye albamu yao iliyofanya vizuri sana mwaka 1992 ya "Totally Krossed Out."
Wawili hao walishangaza mashabiki kwa ukomavu wao katika rapu, ingawa wimbo huo uliandikwa na Dupri.
No comments:
Post a Comment