PAPA FRANCIS AKIRI KUPITIWA NA USINGIZI WAKATI IBADA IKIENDELEA...

Papa Francis I wakati wa Ibada hiyo.
Papa Francis amekiri kusinzia wakati akisali mwishoni mwa siku ndefu, lakini alisema anafikiri Mungu 'ameelewa'.

Baba Mtakatifu huyo alikuwa amesimama mbele ya watu 200,000 waliokusanyika pamoja kwenye Viwanja vya Mtakatifu Petro pale alipotoa maoni ambayo hayakupangiliwa kuanzia kutoka kumbukumbu za bibi yake, uamuzi wake wa kuwa Padri na rushwa katika siasa.
Akisababisha vicheko kutoka kwa umati huo, alifafanua jinsi anavyosali kila siku mbele ya madhabahu kabla ya kwenda kulala.
"Wakati mwingine nalala, kazi hiyo ngumu ya siku hukufanya ujikute umelala, lakini Mungu anaelewa," alisema.
Akiwataka Wakatoliki kuongeza juhudi kusaidia mafukara na wenye mahitaji katika jamii alisendelea: "Kama tukijitoa, tutakuta umasikini.
Leo, inaniuma kuzungumzia, kukutana na mtu asiye na makazi ambaye amekufa kutokana na baridi, sio habari.
"Leo, habari ni kashfa, hiyo ndio habari, lakini hao watoto wengi ambao hawana chakula - hiyo sio habari.
"Hili ni kaburi. Hatuweza kubweteka kirahisi tu wakati mambo yakiwa namna hii."
Miongoni mwa umati huo, ambapo wengi wao tayari wanajihusisha na kazi za kujitolea, walimkatiza mara kwa mara kwa makofi.

No comments: