Dk Willibrod Slaa. |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuanzia sasa kitatumia utaratibu mpya wa kuwapata wagombea wa uongozi ndani ya chama hicho, ambapo watatangaza nafasi katika magazeti ili wanaotaka waombe.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alisema hayo jana wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa, pamoja na jinsi mchakato wa Katiba mpya unavyoendelea.
Kuhusu utaratibu huo, alisema Chadema kimekua na ili kupata uongozi ndani ya chama hicho, kutakua na kipindi kirefu cha kuwaangalia na kuwafuatilia wagombea, lengo likiwa ni kusimamia uadilifu.
“Chadema imekua na leo ina miaka 20 na inajifunza, sasa je, endapo ikichukua watu dakika ya mwisho inakuwaje…Chadema ya leo haipokei makapi kwa sababu utaratibu unaotarajiwa kuanza sasa, ni kutangaza nafasi za wagombea kwenye magazeti, ili wanaotaka waombe,” alisema Dk Slaa wakati akijibu swali lililohusu kama chama hicho hakipokei makapi.
Alisema chini ya utaratibu huo wanataka wagombea wasije dakika ya mwisho, kwani ubunge sio karanga na watakuwa na kipindi kirefu cha kuwaangalia, kuwapima na kuwafuatilia kazi zao ili kujua uadilifu wa mhusika awapo jukwaani kwani wapo wanaoingia bungeni kwa fedha.
No comments:
Post a Comment