MWANASHERIA WA KIKE ALIYESHITAKIWA KWA KUFANYA UKAHABA NAYE AWASHITAKI WENZAKE...

Reema Bajaj.
Mwanasheria mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza picha zake za utupu.

Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama 'John Doe' walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.
Sasa wateja, wazee wa mahakama, na majaji wote wameshayaona makabrasha hayo ya kuaibisha, Bajaj anasema. Ana 'hasira mno, huzuni, aibu, na fedheha,' kwa mujibu wa hati yake ya mashitaka, ambayo ilisambazwa katika mtandao na gazeti la Illinois la the Daily Chronicle.
Johnson na Campbell, ambao sasa wana changamoto yao pamoja, hawakujibu simu mara moja walipotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hati hiyo ya mashitaka.
Bajaj alipatikana na hatia ya ukahaba wakati wa majira ya joto. Alipigwa faini ya Dola za Marekani 2,500 na kutakiwa kufanya kazi za kujitolea kwa jamii masaa 50.
Polisi walimkamata Bajaj mnamo Juni 2011, wakisema wamegundua baruapepe kati yake na mwanaume ambaye alimlipa kwa ajili ya kufanya naye ngono kama sehemu ya uchunguzi kwenye kesi isiyohusiana, imeripotiwa. Alitiwa hatiani kwa makosa matatu uya ukahaba, lakini mawili yalitupiliwa mbali.
Polisi walisema hakukuwa na uhusiano wowote kati ya ukahaba wake na wateja wa kampuni yake ya uwakili. Katika hati yake ya mashitaka aliyowasilisha Jumatatu, Bajaj alisema anahofia picha hizo na maelezo kwamba zilidaiwa kusambazwa baada ya kukamatwa kwake zinaweza kuathiri biashara ya kampuni yake.
Alikuwa na changamoto yake binafsi, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za habari. Tovuti ya kampuni yake ya uwakili kwa sasa haifanyi kazi.
Kabla ya kushitakiwa kwa ukahaba, Bajaj alijitolea muda wake katika Ofisi ya Utetezi wa Jamii Boone County, iliripoti Rockford Register baada ya kukamatwa kwake.

No comments: