Mtangazaji huyo akinyonya maziwa ya mama. |
Mtangazaji wa Televisheni ya Uholanzi amewaacha midomo wazi watazamaji baada ya kunywa maziwa moja kwa moja kutoka kwenye matiti ya mam mmoja wakati wa kipindi chake cha wakati wa kipekee Jumamosi usiku.
Mwongozaji kipindi, Paul de Leeuw alikuwa amealika kundi la wanawake kutoka asasi moja ambayo inaruhusu kubadilishana maziwa ya mama kati ya akinamama kwenye kipindi chake cha burudani, Langs de Leeuw.
Wakati wa mahojiano na wanawake hao, mwongozaji huyo aliuliza kama maziwa ya mama yalikuwa 'mazuri na matamu' na kuomba kama anaweza kuonja kidogo.
"Sawa, kama hung'ati unaweza kujaribu," aliyejitolea, akifahamika kama Wendy, alisema.
De Leeuw alijongea na kunywa kutoka kwenye moja ya matiti ya mama huyo kabla ya kuachia na kuhamia kwenye titi la pili.
"Nimegundua la pili lina ladha nzuri zaidi, lakini naweza kupata ladha kwamba amekula boga jana," de Leeuw alikejeli.
Kipengele hicho kimeibua shutuma kali katika mitandao ya kijamii lakini Wendy ametetea mabadilishano hayo yasiyo ya kawaida, akisema ilikuwa 'kwa nia njema'.
No comments:
Post a Comment