Msichana huyo akiwa mbele ya nyumba inayodaiwa ilitumika kufanyia unyama huo. |
Msichana mmoja wa Texas ambaye alikuwa na miaka 11 tu wakati alipobakwa na wanaume 20 kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu mwaka 2010 amebainisha kwamba sasa ni mjamzito wa miezi saba akiwa na umri wa miaka 14.
Kijana huyo anasema baba wa mtoto huyo ni rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 15 na kwamba wamepanga kumlea mtoto huyo.
Uhalifu huo wa kushitusha ulivuta hisia kitaifa pale polisi walipoanza kuchunguza Desemba 2010, baada ya mwanafunzi mwenzake msichana huyo kumweleza mwalimu kwamba aliona katika simu video inayoonesha wanaume wakifanya mapenzi na binti huyo.
Waendesha mashitaka wamesema msichana huyo alishambuliwa kijinsia kwenye matukio yasiyopungua matano na wanaume 20 na wavulana mji wa Kusini-mashariki mwa Texas wa Cleveland, takribani maili 45 kaskazini-mashariki mwa Houston.
Msichana huyo alikuwa na miaka 11 wakati huo wa mashambulio hayo kuanzia katikati ya Septemba hadi mapema Desemba, 2010. Polisi walianza uchunguzi Desemba hiyo hiyo, pale video kwenye simu ya mkononi ilipoweka bayana moja ya mashambulio hayo.
Baada ya wachunguzi kufahamu shambulio hilo la kutisha, msichana huyo alihamishiwa sehemu ya kulelea watoto lakini alitoroka kutoka kwenye kundi lake nyumbani huko Beaumont, Texas Desemba 2011 na akaangukia kwenye shambulio jingine la ngono wakati alipokuwa akiishi mitaani.
Agosti 2012, alirejea mjini Houston kuungana na familia yake.
Sasa anaishi na mama yake, kaka na madada zake.
Mama yake, Maria, alisema kwamba alichanganyikiwa alipogundua msichana huyo alikuwa mjamzito.
"Sawa, pale alipokuja na vipimo vya mimba, nilitamani kusema, 'Toka, potea machoni mwangu, nilichanganyikiwa," alisema.
Mama huyo anasema kwamba kwa sasa amekubali kwamba hii inaweza kuwa sehemu ya tiba ya binti yake.
"Nadhani ni kawaida mno kwamba wakati fulani wasichana, pale inapowatokea kama hivi, wanajaribu kutafuta faraja kwa mtu fulani, kama vile wanataka kujisikia wanapendwa."
Mwathirika huyo, ambaye hakutajwa majina yake, alisema anajisikia fahari kuhusu ujio wa mtoto wake. Pia alisema anatumaini kwamba watu hawatamhukumu kwa kuwa na mtoto nje ya ndoa.
Watuhumiwa wote sita watoto na sita kati ya wakubwa 14 walioshitakiwa wamepatikana na hatia.
Msichana huyo alielezea mfululizo wa mashambulio hayo ya kutisha kwamba yalifanyika katika jamii ndogo Texas ya Cleveland wakati wa kesi dhidi ya Eric McGowen.
Alitoa ushahidi kwamba McGowen alimchukua hadi nyumba moja mnamo Oktoba 2010 ambako alifanya mapenzi na wanaume kadhaa.
Msichana huyo alisema aliingizwa kwenye kile alichokielezea kama 'chumba cha mtoto' katika nyumba hiyo, na kwamba McGowen na wengine walirudia-rudia kufanya naye mapenzi.
Binti huyo aliangua kilio pale waendesha mashitaka walipoonesha video yake akifanya mapenzi kinyume cha maumbile wakati wa moja ya mashambulio hayo.
Alimtambua McGowen katika video hiyo akicheka kwa nyuma, akiwahimiza washambulizi kuchangamkia ngono na binti huyo.
McGowen alikiri kumbaka msichana huyo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 99 jela mwaka 2012.
Mshitakiwa Jared Len Cruse pia alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kushiriki ubakaji.
No comments:
Post a Comment