Mandhari ya mji wa Arusha. |
Hatima ya wagombea wa udiwani Jimbo la Arusha Mjini, inatarajiwa kujulikana Mei 8 mwaka huu, baada ya Kamati ya Siasa ya Mkoa kutoa majina ya wagombea katika kata hizo nne.
Mchakato wa kura za maoni kupata wagombea
udiwani wa kata nne za Jiji la Arusha ndani ya CCM, uliofanyika Mei 2 mwaka huu, na wagombea walioshindwa wamekubaliana na matokeo na wameahidi kutoa ushirikiano kwa wataopitishwa katika vikao vya juu vya chama.
Akizungumza na mwandishi jana, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha, Allani Kingazi alisema kura za maoni ni sehemu tu ya machakato wa awali wa kuelekea uteuzi wa vikao vya juu na kikao cha mwisho ni Kamati ya Siasa ya Mkoa na sio vinginevyo.
Kingazi alisema kushinda katika kura za maoni, sio ushindi wa kuwa mmoja wa wagombea wa chama, bali itazingatiwa vitu vingi ikiwemo sifa za mgombea kwa jamii na uadilifu ndani ya chama na nje ya chama.
Katika Kata ya Kaloleni, waliojitokeza kutaka kuwania na kura zao kwenye mabano ni pamoja na Abdallah Mohamed (16), Emmanuel Meliali (42),
Iddy Mkuluu (25), Hassani Sharifu (4) na Felix Mrosso aliyejitoa lakini alipigiwa kura 4.
Katibu Kingazi alisema kutokana na msimamo huo chama ngazi ya kata kilimpendekeza Meliali kuwa mgombea wa udiwani wa kata hiyo kwa kuongoza na kupata kura 42 kati ya kura 87 zilizopigwa.
Alisema katika Kata ya Kimandolu kura zilipigwa 102 na wagombea walikuwa wawili Shija Kasanzu
na Edna Saulina. Kasanzu alijitoa na Edna alipata kura zote 102 na kupendekezwa kuwania udiwani wa kata hiyo.
Kata ya Elerai wagombea walikuwa watatu, kura zilizopigwa zilikuwa 100 na chama ngazi ya kata kilipendekeza Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Elerai, Emmanuel Laizer aliyepa kura 82 kuwa mgombea.
Mwalimu huyo aliwabwaga wapinzani wake Peter
Kasela maarufu kwa jina la 'majeshi’ aliyepata kura 14 na Losioki Laizer aliyeambulia kura 4.
Kata ya Themi aliyependekezwa na chama ni Lobora Ndaruvoi, alipata kura 44 na kuwaangusha wapinzani wake Victor Mkolwe aliyepata kura 38 na Muhidini Kanoni, aliambulia kura 11.Kura 93 zilipigwa.
No comments:
Post a Comment