KUSHOTO: Moshi ukifuka kwenye moja ya injini za ndege hiyo angani. KULIA: Mafundi wakiichunguza injini hiyo mara baada ya kutua Uwanja wa Heathrow. |
Abiria mmoja ameelezea jinsi 'moto mkubwa'
ulivyokuwa ukionekana kutoka ndani ya ndege ya British Airways kabla kwa
namna ya ajabu kulazimisha kutua kwa dharura kwenye Uwanja wa Heathrow
jana.
Ndege hiyo aina ya Airbus A319, ambayo ilikuwa imebeba abiria 75 katika safari yake kuelekea Oslo, ililazimika kurejea uwanjani hapo muda mfupi baada ya kuruka sababu ya 'hitilafu ya kiufundi', British Airways imesema.
Picha za ajabu kutoka eneo la tukio zinaonesha moshi ukifuka kutoka kwenye ndege hiyo huku ikiwa bado angani na mashuhuda wameelezea kusikia 'mlipuko' na kuona moja ya injini zake ikiwaka moto wakati ikiruka juu.
Tetesi zimeeleza kwamba ndege hiyo ilishambuliwa na ndege warukao angani, ingawa hakukuwa na uthibitisho wowote rasmi kuhusiana na hilo.
Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Heathrow alisema abiria wote wametolewa wakiwa salama.
Msemaji huyo alisema uwanja huo ulibaki wazi wakati wote wa tukio hilo. Njia zote za kuruka/kutua zililazimika kufungwa jana asubuhi lakini baadaye zikafunguliwa na kwamba ndege hiyo inafanyiwa uchunguzi.
Maofisa wametupilia mbali hisia za ugaidi na wachunguzi sasa wanaangalia uwezekano wa ndege kutumbukia kwenye moja ya injini hizo muda mfupi baada ya kuruka.
David Gallagher, ambaye alikuwa abiria kwenye ndege hiyo kueleka Oslo, alisema 'moto mkubwa' ulikuwa 'ukionekana wazi' kutoka ndani ya ndege.
Gallagher alisema: "Kwa takribani dakika nane au tisa ndani ya ndege hiyo kulikuwa na milio mikubwa ikirindima, sio mlipuko lakini wazi haikuwa milio wa kawaida."
Abiria hao waliohamishiwa kwenye ndege nyingine uwanjani hapo walitahadharishwa kutarajia kuchelewa kwa dakika kati ya 30-60 kutokana na kukamilisha taratibu za ndege hizo.
Tukio hilo linachunguzwa na Tawi la Uchunguzi wa Ajali za Ndege.
No comments:
Post a Comment