KUSHOTO: Sehemu yalipotokea mauaji hayo. KULIA: Muhammed Saleem Chaudhry. |
Babu amechomwa visu na kufa hatua chache kutoka mlango wa nyumba yake wakati akirejea nyumbani hapo kutoka kwenye sala ya jioni msikitini.
Muhammed Saleem Chaudhry, miaka 75, alikutwa katika dimbwi na majirani zake ambao waligutushwa na kelele za maumivu.
Alichomwa visu mara tatu mgongoni na kupigwa kichwani wakati wa shambulio hilo lililotokea Jumatatu usiku.
Juzi familia yake iliyoumizwa ilieleza huzuni yao kutokana na kumpoteza 'mzee wao huyo', huku polisi wakihaha kugundua sababu za shambulio hilo la kutisha.
Majirani walisema eneo hilo limekumbwa na upepo wa makundi ya wahuni.
Baba huyo wa watoto saba 'anayeheshimika mno' - ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa baridi yabisi na kutembea kwa msaada wa fimbo - hafikiriwi kuwa alilengwa kwa tukio la uporaji ulioshindikana sababu pochi yake ilikutwa kwenye mavazi yake.
Maofisa walisema wameondosha uwezekano wa babu huyo wa wajukuu 22 alikuwa muathirika wa shambulio la kibaguzi, na kuwa huenda alikuwa akifuatiliwa kwa umbali fulani au wakati wote wa safari hiyo ya nusu maili kutoka msikitini kwake, lakini hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha hisia zozote kati ya hizo.
Alishambuliwa mkabala na shule moja ya msingi majira ya Saa 4:30 asubuhi, baada ya kumaliza sala ya jioni kwenye msikiti wa Green Lane huko Small Heath, Birmingham, ambako alisali mara tano kwa siku.
Chaudhry, mwoka mikate mstaafu, alikuwa akirejea kwa mkewe mwenye miaka 50, Said, ambaye alikuwa amelala wakati huo wa tukio.
Juzi, mmoja wa mabinti wa wanandoa hao, Shazia Khan, miaka 45, alisema: "Wapasuaji walimweleza mama yangu hawajawahi kuona majeraha ya kuchomwa visu ya kutisha kama hayo hapo kabla.
"Alikuwa ameshambuliwa majira ya jioni kivyake. Kwangu inaonekana yamedhamiriwa. Nimehuzunishwa mno."
Kaka yake, Shahid, aliongeza: "Mama yangu amehuzunishwa mno. Dunia yake imesambaratika."
Mpelelezi Inspekta Martin Slevin, kutoka Polisi wa West Midlands, alisema: "Tuko katika hatua za awali mno za uchunguzi huu na sababu za shambulio hilo bado hazijafahamika.
"Leo tutakuwa tukichunguza picha za kamera ya CCTV na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo ambao wanaweza kuwa waliona kitu fulani usiku wa jana.
"Hakika tunataka kusikia kutoka kwa kila mmoja ambaye alikuwa kwenye eneo hilo wakati huo na kuona chochote kile."
No comments:
Post a Comment