WASICHANA WADOGO 13 WACHANGAMKIA 'NGONO YA VITA TAKATIFU'...

Askari walioasi nchini Syria wakishangilia moja ya mafanikio yao.
Takribani wasichana 13 wa Tunisia wameripotiwa kusafiri kwenda eneo la Kaskazini mwa Syria linaloshikiliwa na waasi kujitolea kujiuza miili yao kwa wapiganaji wa upinzani.

Ripoti hizo zimekuja huku wito katika Tunisia ukiongezeka kwa amri za kidini au 'fatwa' ambazo zimesambazwa katika mitandao ya intaneti zikiwataka wanawake kushiriki vita takatifu kupitia ngono.
Wiki iliyopita, Waziri wa Tunisia wa mambo ya dini aliwataka wasichana kutokubali kutumiwa na wahubiri wa Kiislamu nje ya Tunisia ambao, imeripotiwa, wamefanikisha 'fatwa kadhaa za ngono'.
Noureddine al-Khadimi amepinga fatwa za 'ngono ya vita takatifu', akiwaasa watu wa Tunisia na taasisi za serikali kuzipuuza.
Magazeti ya Tunisia yameripoti kwamba kijana mdogo wa Tunisia alimtaliki mkewe, na kwamba wote walielekea Syria takribani mwezi mmoja uliopita 'kumwezesha mke huyo kushiriki ngono ya vita takatifu na wajahidina' huko.
Ripoti hizi zilifuatia zile za kwanza za video iliyosambazwa sehemu nyingi katika mtandao wa intaneti na tovuti za kijamii nchini Tunisia zikionesha wazazi wa msichana aliyefichwa kwa mtandio anayeitwa Rahmahat, mwenye umri wa miaka 17.
Walisema Rahmahat alitoweka nyumbani asubuhi moja na 'baadaye waligundua kwamba alielekea nchini Syria kufanya ngono ya vita takatifu.'
Msichana huyo mdogo amesharejea katika familia yake, ambayo imemficha kutoka macho ya watu, na kusema kwamba binti yao sio mshikadini sana ' ila alishawishiwa na wanafunzi wenzake ambao wanafahamika kwa ukaribu wao na Salafist wa vita takatifu.'
Wazazi wake walisema hawa wanafunzi wenzake wanaweza kuwa walimrubuni na kumshawishi kusafiri kwenda nchini Syria 'kuwasaidia wajahidina kule.'
Habari kama hizo zimekuwa maarufu nchini Tunisia na wazazi wanafahamu kuhusu mchango wa viongozi wa Kiislamu wenye kipaji katika nchini nyingine za Kiarabu unaweza kuwatawala watoto wao.
Matamko hayo ya waziri yamekuja baada ya kuzagaa huko kwa fatwa ya 'ngono ya vita takatifu' katika mtandao wa intaneti ikiwaalika wasichana wadogo kusaidia wapiganaji [upinzani] nchini Syria kwa kujitolea huduma za ngono kwenye uwanja wa mapambano.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Tunisia ambavyo vimewanukuu wajahidina waliorejea nchini Tunisia baada ya kushiriki katika vita takatifu nchini Syria, wasichana 13 walielekea kwenye uwanja wa mapambano kuitikia fatwa ya 'ngono ya vita takatifu'.
Tovuti za habari na mitandao ya kijamii nchini Tunisia imesambaza fatwa kwa heshima ya Shekhe Mohamed al-Arifi ambayo aliwataka 'wanawake Waislamu' kushiriki vita takatifu kupitia ngono.
Hatahivyo, vyanzo vya habari zilivyo karibu na Shekhe huyo vimekanusha kwamba alitangaza fatwa, vikisisitiza kwamba yeyote ambaye anasambaza au kuamini ni kichaa.
Saudi Arabia inafahamika kwa mapana kuwa inafadhili waasi hao wa Syria wanaipigana Kaskazini mwa Syria na ambao kiini chao 'Salafist' mwelekeo wa Kiislamu kinasaidia idadi kubwa ya wapiganaji vijana - wengi wao wakiwa 'watu wa vita takatifu' na wanatokea pande zote za dunia, ikiwamo Uingereza.
Chini ya sheria ya Kiislamu, mwanaume anaweza kuoa na kukamilisha ndoa kwa ngono na mkewe, kabla ya kumtaliki siku inayofuata bila kipingamizi chochote kutoka kwa mke au familia yake kwa kufuata tu taratibu za dini.
Noor Eddin al-Khadimi, alisema kwamba Watunisia wasijifunge na sheria hiyo ya fatwa.
Wito wake huo uliungwa mkono pia na wapinzani wa nchini Tunisia.
Salma al-Raqiq, mkongwe wa upinzani nchini Tunisia, alisema kwamba 'ndoa hizo za vita takatifu' ni matusi kwa watu wa Tunisia.
Alizitaka pia mamlaka kuanza kushughulika na ongezeko la mtindo wa Watunisia wafuasi wa vita takatifu wanaoelekea nchini Syria kuungana na makundi ya Waislamu wenye siasa kali.
Al-Raqiq alisema kwamba mwenendo huo ni wa hatari mno. Alisema kwamba wasichana wadogo wamekuwa akipelekwa nchini Syria 'kuolewa' na wana-jihad hao kwa masaa machache.

No comments: