MWILI WA ASKARI WAKAA KWENYE GARI NJE YA BAA MIEZI MINNE BILA KUGUNDULIKA...

Baa ambako mwili wa O'Brien ulikutwa baada ya miezi minne.
Mwili wa mwanajeshi wa zamani umelala bila kugundulika ndani ya gari lililoegeshwa kwenye baa kwa miezi minne licha ya majaribio kadhaa ya mmiliki wa eneo hilo kutaka gari hilo liondolewe.

Paul O'Brien, kutoka Cambridge, ambaye alipigana katika Vita vya kwanza vya Ghuba na kutumikia ziara mbili huko Ireland ya Kaskazini, alikutwa nyuma ya gari hilo baada ya kuwa kafungashwa na halmashauri hiyo.
Mwanajeshi huyo mwenye miaka 42, ambaye wakati fulani alibeba mwili wa rafiki yake mkubwa kwa maili tano baada ya kuuawa kwenye kikosi cha upelelezi nchini Ireland ya Kusini, ameelezewa kama 'mtu mkarimu.'
Gari la rangi ya damu ya mzee lilikuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari ya baa ya Lazy Otter, karibu na Stretham katika Cambridgeshire Fens kutoka Oktoba hadi mwishoni mwa Februari.
Lakini licha ya simu za mara kwa mara kutoka kwa mmiliki wa baa hiyo kwenda polisi, hakuna aliyefika kulitazama.
"Ilikuwa mshituko mkubwa kwetu sote kubaini kwamba mwili wake umekuwa katika gari wakati wote huo na ni huzuni mno," alisema Annette Gwinnett, mmiliki wa Lazy Otter.
"Masikini familia yake ingeweza kuwa naye karibu mapema kama polisi wangeshughulikia simu zangu na kuweka kila kitu pamoja.
"Isingeweza kuzuia msiba huo kutokea lakini ni lazima itakuwa imewaumiza kwa wao kutofahamu nini kilichomtokea kwa miezi minne."
Annette alisema alijaribu kuwapigia simu polisi hao mara tatu kuwaeleza kuhusu gari hilo lililoegeshwana pia kujaribu kupiga simu ya mkononi iliyokuwa kando ya gari hilo,  lakini haikujibiwa.
"Lilikuwa ni gari la kibiashara hivyo nilikuwa na mashaka mno pale ilipokosa mtu wa kupokea kwa muda mrefu kama huo," alisema. Tulijaribu na kujaribu na mwishowe simu ikazima.
"Kisha tukawaita tena polisi na walisema ilikuwa eneo binafsi na sio tatizo lao na kutueleza kuwapigia halmashauri.
"Kama tusingekuwa tumefanya hivyo gari hilo lingeweza kuendelea kukaa pale na familia hiyo isingefahamu nini kilichotokea. Tulifanya kila tulichoweza. Ni huzuni sana."
Msemaji wa Halmashauri ya South Cambridgeshire alithibitisha gari hilo liliondolewa na mkandarasi wake Charlton Autoparts mjini Thriplow, karibu na Sawston, Februari 25.
Terry Charlton, ambaye anamiliki Charlton Autoparts, alisema: "Ni mimi niliyegundua mwili huo na ilikuwa haipendezi na kukatisha tamaa kama unavyoweza kufikiri."
Mazishi ya O'Brien yalifanyika karibu na Newcastle Machi 13. Marafiki zake walikesha kwenye baa ya Lazy Otter kwa kile kinachoweza kuwa siku yake ya kuzaliwa siku mbili baadaye.

No comments: