ABIRIA VIBONGE WAANZA KUONJA MAKALI YA NAULI ZA NDEGE...

Abiria kama huyu sasa wameanza kupata karaha ya nauli mpya kwenye ndege.
Ndege za Samoa zimeanza rasmi kuwatoza abiria kwa kiti kufuatana na kiasi cha uzito alichonacho.
Chini ya mfumo mpya abiria wanalipa bei moja kwa kilo kwa bei ya tiketi, ambayo inatofautiana kutegemeana na urefu wa safari.

Mkuu wa Shirika la Ndege la Samoa, Chris Langton alieleza kwamba ni 'njia ya haki ya kusafiri.'
Chini ya utaratibu wa malipo kulingana na uzito abiria wanaingiza uzito wao kwenye sehemu ya kukata tiketi mtandaoni katika tovuti ya Shirika la Ndege za Samoa.
Viwango vya nauli vya Ndege za Samoa ni kati ya Dola za Marekani 1 hadi takribani Dola za Marekani 4.16 kwa kilo imeripotiwa.
"Kwa kawaida watu wamekuwa wakisafiri kwa msingi wa viti lakini wengi wa wasafirishaji wa anga wanaelewa kwamba ndege haziendeshi kwa kufuata kiti bali kufuatana na uzito na hasa ndege ndogo uko kwenye kiwango kidogo unachoweza kukubaliwa kwa masharti ya  tofauti ya uzito kati ya abiria," alisema Langton.
Langton alisema kwamba familia zinazosafiri na watoto sasa ziikuwa zikilipa nauli nafuu.
"Hakuna ada ya ziada kuhusiana na mzigo unaoongezeka au kitu kingine - ni kilo tu kilo ni kilo," alisema.
Abiria wanaweza pia kuongeza uzito wa mizigo yao - hakuna ada tofauti sababu ya mzigo wa ziada.
Ndege za Samoa zinafanya safari za ndani na kuelekea Samoa nchini Marekani - inadhaniwa kwamba uamuzi huo unaweza kuhamasisha mashirika mengine ya ndege kuanzisha sera kama hizo.
Viti vya ndege vinakuwa kufuatana na mahitaji na mwaka jana Airbus ilitangaza kwamba itaweka viti vyenye upana wa ziada kwa ajili ya abiria wenye uzito mkubwa huku idadi ya abiria wenye unene uliopitiliza ikizidi kuongezeka.
Theluthi moja ya idadi ya watu kwa sasa ni wenye unene uliopitiliza, wanaokadiriwa kufikia asilimia 42 ifikikapo mwaka 2030.
Viti viwili vyenye ukubwa wa inchi 20 vitawekwa katika kila upande wa njia za ndani ya ndege, ikitoa nafasi kwa viti vyenye ukubwa wa kawaida wa inchi 18 ndani ya ndege ya A320 - katika ndege aina ya Boeing kwa kawaida viti vina ukubwa wa inchi 17.
Abiria wenye maumbo makubwa zaidi watakuwa na uwezo wa kununua viti vye ukubwa wa ziada kwa gharama ya ziada, ambayo inatarajiwa kuthibitisha faida katika sekta ya usafiri wa anga.
Mashirika ya ndege yataingiza hadi Dola za Marekani milioni 3 zaidi katika faida kwa zaidi ya kipindi cha miaka 15 kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Huffington Post.

No comments: