MWANAUME ATIMULIWA KWENYE TAMASHA SABABU NI MZURI MNO...

   
Intaneti imejawa na tetesi kwamba huyu ni mwanaume ambaye ametimuliwa nchini Saudi Arabia kwa kuwa ni anavutia mno.

Omar Borkan Al Gala, mshairi, mwigizaji, na mpigapicha kutoka Dubai, anaripotiwa kuwa mmoja wa wanaume watatu walienguliwa kutoka kwenye tamasha mjini Riyadh mapema mwezi huu na polisi wa kidini katika kulinda himaya hiyo ya Kiislamu.
Kamisheni ya Promotion of Virtue and Prevention of Vices nchini Saudi - ambako sheria kali zinadhibiti mahusiano kati ya wanaume na wanawake ambao hawahusiani - imewatimua wanaume hao na kuwarejesha Abu Dhabi kwa tahadhari kwamba wanawake wanaweza 'kuwatamani kimapenzi'.
Ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la Kiarabu la Elaph inayosema: "Maofisa wa tamasha hilo walisema watu hao watatu kutoka Emirati walioondolewa kwenye viwanja hivyo walikuwa wanavutia mno na kwamba wafanyakazi wa Kamisheni hiyo walihofia wanawake wanaotembelea tamasha hilo wanaweza 'kuwatamani kimapenzi.'
Utambulisho wake uliwekwa hadharani na Jezebel ambalo liliripoti kwamba amerejeshwa kwao Umoja wa Falme za Kiarabu.
Ingawa bado haijathibitishwa kwamba alikuwa miongoni mwa wanaume hao, Al Gala ametuma taarifa kwenye ripoti halisi katika ukurasa wake wa Facebook, sambamba na taarifa kama: "Urembo wa mwanamke lazima uonekane kutoka katika macho yake, sababu hiyo ni njia ya kwenda moyoni mwake, mahali ambako mapenzi yanaishi."
Ukurasa wake wa Facebook umepambwa na picha zake katika pozi mbalimbali ambazo Al Gala anaonekana kajiandaa katika kamera - inaonekana kama amevalia vitu vyeusi machoni.
Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Al Gala alipata wafuasi 139,616 waliopenda na takribani 36,487 wakimzungumzia.
Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu umetoa taarifa rasmi ikionesha kwamba polisi wa kidini walizingatia kuhusu uwepo usiotarajiwa wa mwanamke wa kike ambaye hakutajwa katika eneo hilo kwenye Jenadrivah Heritage and Culture Festival.

No comments: