HILI NDILO JIJI HATARI ZAIDI KUISHI HAPA DUNIANI...

Baadhi ya ndugu wakiuguza wapendwa zao walioathirika na vurugu za jijini San Pedro Sula.
Jiji la San Pedro Sula nchini Honduras linaongoza orodha ya maeneo yenye vurugu zaidi duniani katika sayari hii, ambako misiba, ukatili na vifo vya mauaji ya halaiki vinazidi kutapakaa.

Takribani matukio matatu ya mauaji huripotiwa kila siku katika taifa hilo linalosafirisha kwa wingi kahawa nje, mengi kati ya hayo katika mikono ya magenge na wakiritimba wa dawa za kulevya ambao wanaendesha biashara hiyo kwa uhuru kwenye eneo lisilo na sheria, fukara na lenye uozo katika mfumo wa kisheria.
Watu wenye silaha za kivita wanashikilia maeneo ya ovyo na vijiji, wakifahamu vema kwamba polisi hawawajibiki ipasavyo na ni walarushwa wakubwa.
Orodha hiyo ya miji yenye vurugu zaidi ilikusanywa na Citizen Council for Public Security, Justice and Peace, shirika lenye makazi yake nchini Mexico, likitumia takwimu za uhalifu za mwaka 2012 kutoka Amerika Kaskazini na Kusini.
San Pedro Sula lilikuwa na mauaji 1,218 mwaka 2012 (wastani wa mauaji 3.3 kwa siku). Lilikuwa likifuatiwa na Acapulco nchini Mexico; Caracas nchini Venezuela na Distrito Central nchini Honduras.
Iliripotiwa mwaka jana kwamba San Pedro Sula inazingirwa na moja ya uchumi dhaifu kabisa wa Amerika Kusini - na karibu asilimia 70 ya idadi ya watu wanaishi kwenye umasikini.
Wengi wanaona uhalifu kuwa suluhisho lao pekee. Au wanaondoka, na kufanya safari ndefu na ngumu kuelekea Marekani.
Magenge ya mitaani yanayofahamika kama Maras yamekuwa yakijiingiza kwenye matukio makubwa ya mauaji, huku wasafirishaji wa dawa za kulevya wa Mexico wakinunua ardhi na kuwapa vikosi vyao vya wauaji.
Kwa wote wanaoendesha mgongano wa sheria, mahakama inaweza kuwa mpaka wa mbali.
Karibu nusu ya wafungwa wa nchini humo hawajahukumiwa na wengi wanasubiri kwa miaka kabla ya kusikilizwa mashitaka yao.
Wengine hufa kwenye magereza kwa kuchomwa visu, kupigwa risasi au moto kama ilivyotokea kwa mmoja ambaye alitapakaa kwenye gereza la Comayagua Februari 2012, akiwafungia wafungwa ndani ya selo zao na kuwachomwa moto wakiwa hai.
Uchunguzi uliofanywa mapema mwezi uliopita uligundua kwamba vikosi laghai vya polisi vya mauaji vinafanya kazi bila hofu kote nchini Honduras, wakijichukulia sheria mikononi mwao na kujifanya majaji, mahakama na watekeleza hukumu.
Licha ya msaada wa mamilioni ya dola kutoka Marekani kwa Honduras wenye lengo la kuongeza weledi kwa polisi wa nchi hiyo, imefahamika katika miaka mitatu iliyopita, waendesha mashitaka wa Honduras wamepokea malalamiko rasmi hadi 150 kuhusu vifo vya mtindo wa vikosi vya mauaji katika mji mkuu wa Tegucigalpa, na takribani 50 zaidi katika kitovu cha uchumi cha San Pedro Sula.
Chuo Kikuu cha Taifa Huru cha nchini humo, kilenga ripoti za polisi, kimehesabu raia 149 waliouawa na polisi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wakiwamo wafuasi 25 wa genge mashuhuri la mtaa wa 18.
Polisi kwa muda mrefu wamekuwa wakishutumiwa kwa kufanya kazi zaidi kama wauaji kuliko maofisa wa kusimamia sheria nchini Honduras, lakini kesi chache hazijawahi kabisa kuchunguzwa.
Katika mwaka uliopita, polisi walidaiwa kuhusika katika vifo vya mwandishi maarufu wa redio nchini Honduras na mtoto wa kiume wa mkuu wa zamani wa polisi - lakini hakuna mauaji yoyote kati ya hayo yamepatiwa ufumbuzi.
Hata mkuu wa polisi wa nchini humo ameshitakiwa kwa kula njama.
Mnamo 2002, ripoti ya polisi ya mambo ya ndani ilimtuhumu mkaguzi wa polisi wa magereza wa wakati huo, Juan Carlos Bonilla kwa matukio matatu ya mauaji - na kumhusisha kwenye vifo 11 zaidi na utoweshwaji ambao ulisemekana ulikuwa sehemu ya sera za polisi za 'kusafisha jamii.'
Alijaribu na kuachiliwa kwenye moja kati ya mashitaka hayo matatu. Mkuu wa kitengo cha mambo ya ndani ambaye aliandaa ripoti hiyo, Maria Luisa Borjas, alitimuliwa kutoka kwenye idara hiyo, na kesi zilizobakia, kama uhalifu mwingi nchini Honduras, haukuchunguzwa.
Mwaka jana, Bonilla alichaguliwa kuongoza kikosi cha taifa cha polisi licha ya maswali ambayo hayakujibiwa kuhusu yaliyomtokea siku za nyuma.

No comments: