AWA MWANAMKE WA KWANZA KUONGOZA SALA BAADA YA MIAKA 183...

Jean A. Stevens (kulia) akiendesha sala mbele ya maelfu ya waumini wa Mormoni.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 183, mwanamke ameongoza sala Jumamosi kwenye mkutano wa nusu ya mwaka wa Kanisa la Jesus Christ of Latter-day Saints.

Jean A. Stevens aliongoza ibada ya kufunga kipindi cha sala ya asubuhi kwa zaidi ya wa-Mormoni 100,000 waliokusanyika huko Salt Lake City kwa siku mbili za mkutano mkuu, na mamilioni wengine wakitazama kupitia satelaiti, redio au matangazo ya intaneti.
Pamoja na majukumu mengine ya kanisa, Stevens ni mjumbe wa bodi ya watu watatu ambayo inashauri na kusaidia wazazi katika kuwafunza watoto wao kuhusu kanisa hilo, ambalo lina zaidi ya wafuasi milioni 14 kote duniani.
Mtetezi wa kundi la nadharia na haki ya usawa wa wanawake alizindua kampeni mapema mwaka huu akiwataka viongozi wa kanisa kuruhusu wanawake kuongoza ufunguzi na ufungaji wa sala - wa kwanza kwa mkutano huo - kama ishara ya usawa wa kijinsia.
Wanawake hushika nafasi za uongozi katika kanisa hilo la Mormoni lakini hawaruhusiwi kuwa maaskofu au marais wa taasisi hiyo, ambayo maeneo ya kijiografia yanafanana na yale ya Majimbo Katoliki.
Kwenye mikutano ya zamani, wanawake wamekuwa mara chache wakipewa risala na kuweza kuongoza sala katika mikusanyiko.
Kampeni hiyo ya 'Waache Wanawake Waongoze Sala' ilizinduliwa Januari kutoka katika kundi hilohilo ambalo limevuta hisia kitaifa Desemba kwa kuwaasa wanawake kuvaa nguo za ndani wakati wakienda kanisani badala ya sketi au nguo kuvuta hisia kuhusu kinachoonekana kama kukosekana usawa wa kijinsia ndani ya utamaduni Mormoni.
Amber Whiteley, mwenye miaka 23, kutoka St. Louis, alikuwa mmoja wa waratibu wa kampeni hiyo na alisema Jumamosi 'alisisimuliwa' na kushindwa kujizuia kutabasamu pale aliposikia habari hizo.
"Nafikiri inaonesha kwamba ilikuwa hakika huruma kwa niaba ya kanisa ... kwamba wanawake ni muhimu mno katika kanisa na kwamba sauti za wanawake zina umuhimu," alisema Jumamosi.
Pia inaonesha kwamba 'sala za wanawake zina umuhimu kuzidi za wanaume," alisema Whiteley.
Msemaji wa kanisa Eric Hawkins alisema viongozi wa Mormoni mwishoni mwa mwaka jana waliamua atakayekuwa akiongoza sala za mkutano mkuu, ambapo ilikuwa kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ya sala za wanawake.
Hawkins hakufafanua sababu za kuteuliwa kwa Stevens, lakini alisema viongozi wa kanisa hilo ndio waliochagua kumpa wito huo na baraka.
Mapema Jumamosi, Thomas S. Monson, rais wa imani hiyo, alitangaza kanisa hilo linapanga kujenga makanisa makubwa mapya mawili, mjini Rio de Janeiro na Cedar City, Utah.
Makanisa hayo ni mahususi kwa Watakatifu wa Siku Zijazo na yanatumiwa kwa tambiko za kidini ikiwamo ubatizo, sherehe za ndoa na kanuni nyingine zenye lengo la kuimarisha mafundisho ya kanisa.
Mahali yatakapojengwa majengo hayo mapya patatangazwa baadaye, lilisema kanisa hilo. Duniani kote kuna makanisa 141 yanayoendesha ibada na 29 yanayoendelea kujengwa.
Kanisa jipya lililotangazwa kujengwa mjini Rio de Janeiro litakuwa la nane katika mipango au makanisa yanayoendesha ibada nchini Brazili, ambako kuna zaidi ya waumini milioni 1.1 wa Mormoni.
Makanisa sita yanaendesha shughuli nchini humo, na la saba limepangwa kujengwa mjini Fortaleza.
Kwenye mkutano mkuu wa mwisho Oktoba, maofisa wa kanisa walitangaza kupunguza umri wa chini kwa wamisionari: kutoka miaka 21 hadi 19 kwa wanawake, na kutoka 19 hadi 18 kwa wanaume.
Viongozi wa kanisa na walio nje ya uongozi wanaamini kwamba uamuzi huo utafungua milango kwa wanawake wengi zaidi kujitokeza kutumikia misheni.
Kipindi cha nyuma, asilimia 15 tu ya wamisionari walikuwa wanawake.
Hadi kufikia Aprili 4, zaidi ya wamisionari 65,000 wa Mormoni walikuwa wakitumikia kanisa hilo duniani kote, alisema Monson.
Zaidi ya wamisionari 20,000 wa ziada wameitwa kutumikia kanisa hilo, wakati wengine 6,000 wapo katika mchakato wa usaili.

No comments: