MWANAMKE MNENE ZAIDI YU MAHUTUTI HOSPITALINI BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI HATARI...

Georgia Davis (kushoto) akiwa na mama yake.
Mwanamke mwenye zaidi ya kilo 180 anasemekana kuwa mahututi hospitalini baada ya kupata maambukizi jhatari ya ngozi yaliyomwacha akipigania roho yake.

Siku za nyuma akitambulika kama kijana mnene zaidi Uingereza, Georgia Davis, mwenye miaka 20, alilazwa hospitalini huko Merthyr Tydfil, Ijumaa akisumbuliwa na maambukizi kwenye ngozi ya cellutilis.
Georgia anasemekana kuwa katika hali isiyotabirika kwenye wodi ya urejeshaji fahamu, na anahitaji msaada kuweza kupumua.
Stepdad Arthur Treoloar, mwenye miaka 73, alisema: "Tumeelezwa hali ni mbaya - hakika ni mbaya.
"Alilazwa kwenye wodi hiyo Ijumaa na sasa anapumua kwa msaada wa mashine. Tumekuwa tukielezwa hawezi kufanikisha kupumua mwenyewe."
Georgia tayari amepungua takribani kilo 64 katika kipindi cha miezi tisa alichokaa hospitalini, lakini akarejea katika mlo wake usiozingatia afya tangu aliporuhusiwa kutoka hospitali, akiongezeka zaidi ya kilo 16 katika kipindi cha miezi mitano tu.
Maambukizi hayo yanasababishwa na bakteria wanaoingia kwenye ngozi kupitia kujikata au mchubuko wa ngozi, kuhatarisha na kusambaa katika mwili wake wote.
Watu wenye unene wa kupindukia wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi haya kufuatia kuchanika kwa ngozi na kuwa  nyembamba kwenye mikunjo ya mafuta na upungufu wa usambazaji ambao huruhusu bakteria hao kuingia na kusambaa.
Kama maambukizi hayo yataingia kwenye mkondo wa damu yanaweza kusababisha kuambukiza sumu ya kidonda katika damu (sepsis) na kuhatarisha maisha.
Georgia alitawala vichwa vya habari kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15, pale ilipobainika alikuwa akisafiri kwenye Marekani kujiunga na kambi ya vibonge katika jaribio la kupunguza unene wake wa kilo 132.
Alifanikiwa kupunguza kilo 60 katika kambi hiyo, hata hivyo kijana huyo alianza kuongezeka uzito tena pale aliporejea nyumbani kwa wazazi wake wakati baba yake wa kambo alipogundulika kuwa na saratani ya mapafu.
Kijana huyo alikuwa akiagiza kababu hadi 20 kila wiki kutoka dukani na kutafuna chokoleti siku nzima, viazi vya kukaanga na chupa za lita mbili za Coca Cola, hivyo kusababisha uzito wake kupaa hadi kufikia 224.
Kwa namna ya ajabu Georgia alilazwa katika Hospitali ya Prince Charles, huko Merthyr Tydfil, Wales Juni mwaka jana, baada ya kumpigia mama yake simu ya kuogofya kutoka chumbani kwake akimweleza kwamba alikuwa hawezi kusimama.
Ukubwa wa umbile lake uliwafanya wahudumu wa dharura kushindwa kumtoa Georgia chumbani kwake, na hatimaye kulazimika kubomoa kuta za nyumba hiyo.
Iligharimu kiasi kinachokadiriwa kufikia Pauni za Uingereza 100,000 huku wafanyakazi hao wa dharura wakitumia masaa manane kuangusha kuta mbili za nyumba hiyo iliyoko Aberdare, South Wales, kuweza kumtoa kutoka kwenye chumba chake kilichopo kwenye ghorofa ya kwanza.
Hadi wakati huo ambapo wafanyakazi 50 wa timu ya dharura walipovunja kuta na kutoa, Georgia alikuwa hajawahi kutoka chumbani humo kwa takribani miezi minane.

No comments: