ATUPA NDOANA MTONI NA KUMNASA KAKA SHAVUNI BADALA YA SAMAKI....

Kijana huyo akipatiwa matibabu huku fimbo ikiwa bado imenasa shavuni kwake.
Kijana wa Brazili alilazimika kuanza safari ya hatari ya mtumbwi ya siku mbili kupitia Amazon kuelekea hospitali baada ya kaka yake kumnasa na fimbo ya kuvulia samaki usoni kwa bahati mbaya.

Kijana huyo mwenye asili ya Marekani na India ambaye ana miaka 15 alisafiri maili 195 kwenye mto kutoka nyumbani kwao karibu na mpaka wa Colombia hadi mji wa karibu akiwa na fimbo ya kuvulia samaki kwenye shavu lake.
Kijana huyo alikuwa akipiga mbizi katika mto kukamata samaki walionaswa na mtego ndipo kaka yake alipoona pilika ndani ya maji hayo na kutupa fimbo hiyo, iliyomnasa usoni.
Familia ya vijana hao, kutoka kwenye jamii wenyeji wa Pari-Cachoeira kwenye mpaka wa Colombia, ilisafiri kwa siku mbili kwenda hospitali ya jeshi ya São Gabriel da Cachoeira.
Walimbeba kijana huyo aliyejeruhiwa - ambaye jina lake halikuwekwa hadharani - kwa kutumia mtumbwi, na fimbo hiyo ikiwa usoni mwake wakati wote wa safari kupitia katikati ya joto kali la misitu ya mvua.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya mjini humo, kijana huyo alikuwa akizamia kukamata samaki aliyekuwa amenaswa kwenye 'kakuri' - mtego uliotengenezwa kwa fimbo ambao hunasa samaki wanaoogelea uelekeo tofauti na mkondo.
Kaka yake, ambaye pia alikuwa kwenye mto huo, aliona viwimbi kwenye maji na, kudhania kulikuwa na samaki sambamba, ndipo akatupa fimbo hiyo.
São Gabriel da Cachoeira ambako kuna misitu minene ni manispaa katika eneo la kaskazini-magharibi ya Jimbo la Amazonas nchini Brazili. Sio mbali kutoka Ikweta, na hali ya hewa ni ya joto na unyevu.
Eneo hilo lote lina idadi ya watu karibu 41,000 wengi ni watu asilia waliosambaa zaidi ya maili za mraba 42,000 hasa kwenye misitu minene ya mvua.
Wengi wa wakazi wasio wa asili ya eneo hilo ni askari katika jeshi la Brazili, ambao wanatumikia vipindi vya miaka miwili katika jiji la São Gabriel da Cachoeira - eneo la sehemu kubwa ya makao makuu ya kijeshi.
Ilikuwa timu ya madaktari katika hospitali ya ngome ambao walimfanyia upasuaji kijana huyo kuondoa fimbo hiyo baada ya kuwasili Alhamisi.
Kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini hapo.

No comments: