Uhuru Kenyatta. |
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, mgombea wa TNA, Uhuru Kenyatta anaendelea kuongoza kinyang'anyiro cha Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya huku akifuatiwa kwa karibu na mpinzani wake, Raila Odinga wa chama cha ODM.
Hadi kufikia Saa 5:30 asubuhi ya leo, Kenyatta alikuwa amejikusanyia zaidi ya asilimia 54 ya kura zote zilizokwisha kuhesabiwa hadi wakati huo. Odinga alikuwa amepata zaidi ya asilimia 40.
Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hicho wameachwa mbali sana, ambapo hadi kufikia muda huo mgombea aliye katika nafasi ya tatu alikuwa amejikusanyia kura zaidi ya 117,000 tu na hivyo kufanya mbio hizo kubaki za watu wawili.
Tutaendelea kukupatia matokeo ya kura kadri zitakavyotufikia. Endelea kuperuzi ziro99blog.

No comments:
Post a Comment