Kamanda Suleiman Kova. |
Jeshi la Polisi linaonekana kusafishwa na kujisafisha baada ya safari hii askari wake watano watuhumiwa wa uporaji wa Sh milioni 150 za kidhibiti, kutimuliwa kazi.
Fedha hizo ziliporwa na majambazi Kariakoo Dar es Salaam mwaka jana, na kisha askari hao nao kutumia fursa hiyo kugawana hivyo baada ya uchunguzi wakakutwa na hatia ya uporaji huo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hayo jana alipokutana na waandishi wa habari.
Alisema askari hao, ni waliohusika na ukamataji wa watuhumiwa na vielelezo, baada ya majambazi kupora fedha hizo Desemba 14 Kariakoo katika duka la Kampuni ya Artan Ltd, kwenye makutano ya barabara za Mahiwa na Livingstone.
Katika uporaji huo, majambazi watatu wakiwa na pikipiki wakiendeshwa na mmoja wao, walivamia duka hilo na kupora Sh milioni 150, zilizokuwa zikitolewa dukani kwenda benki.
Kamanda Kova alitaja askari waliotimuliwa kazi kwa ‘kugawana kidhibiti’ kuwa ni Sajini Dancan, Koplo Rajab, Koplo Cavin, Koplo Geofrey na Koplo Kawanami.
“Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewatimua kazi askari hawa kutokana na makosa ya kinidhamu yanayotokana na wizi wa zile Sh milioni 150 ambazo zilikuwa kielelezo,” alisema Kamanda Kova.
Alisema askari hao awali walishitakiwa kijeshi kwa mujibu wa taratibu zinavyotaka, kwamba askari yeyote kabla ya kushitakiwa katika mahakama ya kiraia, ashitakiwe kijeshi kwanza na hukumu ikatolewa.
“Sambamba na kufukuzwa kazi baada ya mashtaka ya kijeshi, jalada la uchunguzi limepelekwa kwa Wakili wa Serikali wa Kanda ya Dar es Salaam na ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka), ili kuangalia endapo kuna ushahidi wa kutosha kuwafikisha katika mahakama za kiraia,” alisema Kova.
Siku moja baada ya uporaji huo kufanyika Kariakoo, vyombo vya habari vilitoa taarifa ya baadhi ya askari Polisi kugawana fedha hizo za kidhibiti katika kata ya Jangwani.
Kutokana na taarifa hizo, Kamanda Kova aliunda jopo la maofisa watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi kuchunguza na akaahidi kwamba ikibainika kuwa tuhuma hizo ni za kweli, wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Katika uporaji huo, mtuhumiwa wa ujambazi, Augustino Kayula (24) alifariki dunia chini ya ulinzi wa Polisi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

No comments:
Post a Comment