MTOTO WA MIAKA MINANE AFUNGA NDOA NA MAMA WA MIAKA 61...

Mtoto Sanele (kulia) akiwa na mkewe, Helen mara baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.
Mwanafunzi wa kiume mwenye miaka minane amemuoa mwanamke mwenye miaka 61 kwa sababu mzimu wa babu yake ulimwelekeza kufanya hivyo.
Sanele Masilela alifunga pingu za maisha na Helen Shabangu, ambaye tayari alishaolewa na ni mama wa watoto watano.
Mvulana huyo, anayetokea Tshwane, Afrika Kusini, alisema aliambiwa na mababu zake waliokufa kuoa na familia yake, inahofia utabiri wa adhabu, utagawanyika kwa harusi hiyo.
Walilipa Pauni za Uingereza 500 kwa ajili ya mahari na Pauni 1,000 zaidi kwa ajili ya sherehe, ambayo iliandaliwa ndani ya kipindi cha miezi miwili tu.
Akiwa amevalia bow tie na suti ya rangi ya kijivu, mtoto Sanele, wa mwisho kati ya watoto watano, alivalishana pete mbele ya wageni waalikwa 100 na hata kupigana mabusu na mke wake huyo.
Tayari imeshitusha jamii lakini familia hiyo imetetea sherehe hiyo, ikisema ilikuwa tu ya kimila na si kifungo cha kisheria.
Mama wa Sanele mwenye miaka 46, Patience Masilela alisema: "Hii ni mara ya kwanza hili kutokea katika familia hii.
"Sanele amerithi jina la babu yake, ambaye hakuwahi kuoa kabla hajafariki hivyo alimtaka Sanele kufunga ndoa. Alimchagua Helen sababu anampenda sana.
"Kwa kufanya hivi tumewafanya wakubwa zetu wawe na furaha. Kama tusingefanya mtoto wangu alichoagizwa basi kitu kibaya kingeweza kutokea katika familia.
"Sina tatizo na hili sababu nafahamu ndicho wakubwa zetu walichokuwa wakitaka na itawafanya wafurahi."
Mjane huyo, ambaye anafanya kazi katika kituo cha kuzalisha taka, aliongeza: "Naweza kusema kwamba hii sio makosa.
"Sanele alikuwa sawa na alikuwa mwenye furaha kuhusu sherehe hiyo na ndicho alichokuwa akitaka. Alikuwa na furaha kuoa na kutoamini kilichokuwa kikitokea."
Sanele na mke wake hawakusaini cheti cha ndoa na hawatakiwi kuishi pamoja. Wote wamerejea katika maisha yao ya kawaida.
Sanele jana alisema anatarajia kufunga ndoa inayostahili kwa mwanamke wa rika lake wakati atakapokuwa mtu mzima.
Aliongeza: "Nilimweleza mama yangu kwamba ninataka kuoa sababu hakika nataka kufanya hivyo.
"Nina furaha kwamba nimemuoa Helen - lakini nitakwenda shule na kusoma kwa bidii.
"Nitakapokuwa mkubwa nitamuoa msichana wa rika langu."
Licha ya kuwa mkubwa kutosha kuitwa bibi yake, bi harusi Helen, ambaye watoto wake wana umri wa kati ya miaka 37 na 27, alifurahia maandalizi.
Helen, ambaye pia anafanya kazi katika kituo cha kuzalisha taka, alisema: "Nimeolewa na nina watoto watano niliozaa mwenyewe, lakini nafahamu kwamba hiki ndicho wakubwa walitaka - na sasa wanafuraha.
"Ni ya kimila. Kwa sasa tunacheza, lakini ni ishara kwamba atakuja kuoa siku moja."
Mume wake aliyeishi naye kwa miaka 30, Alfred, mwenye miaka 65, alisema: "Wanangu na mimi tumefurahi.
"Hatuna tatizo na hilo lakini baadhi ya wanajamii walishitushwa."

No comments: