BALOZI WA AFRIKA KUSINI AREJESHWA NYUMBANI KWA KUZURURA UCHI MITAANI...

Lassy Chiwayo.
Balozi Mdogo wa Afrika Kusini nchini China amerudishwa nyumbani baada ya kudaiwa kukutwa akizurura mitaani huku akiwa uchi.
Lassy Chiwayo, mwanasiasa mkongwe ambaye ametumia muda wake mwingi gerezani pamoja na Nelson Mandela, alisitishiwa mkataba wake mjini Shanghai na amerejea mjini Pretoria.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imesema alirejeshwa kwa 'sababu za kiafya', lakini magazeti kadhaa yaliripoti kwamba Chiwayo alikutwa akizurura uchi karibu na nyumbani kwake miezi mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday World, matembezi yake akiwa uchi yalikuwa ya mara kwa mara.
Chanzo cha habari kilisema: "Alikuwa akitoweka kwa siku kadhaa bila kujulikana na aliweza kupatikana akiwa anatembea uchi kuzunguka eneo hilo."
Chiwayo pia aliripotiwa kumshambulia Balozi wa Afrika Kusini nchini China, Bheki Langa katika sherehe rasmi mjini Beijing.
Chiwayo mwenye miaka 44 amekanusha kuwa amerejeshwa nyumbani akisema ni 'zoezi la kawaida' kwa ujumbe kubadilishiwa majukumu.
Ametupilia mbali habari hizo za kuzurura akiwa uchi na kusisitiza mahusiano yake na Dk Langa yalikuwa 'yaliyoshamiri na yenye nguvu'.
"Yote unayosema ni habari mpya kwangu," alilieleza gazeti la Sunday World. "Sina changamoto zozote za kiafya zinazoweza kuhitaji msaada kutoka kwenye idara hiyo."
Huu ni mfululizo wa hivi karibuni kabisa wa majanga yaliyomkumba Chiwayo, baba wa watoto watatu.
Mwezi uliopita, moto uliteketeza nyumba yake mjini Nelspruit katika shambulio linalohisiwa kuwa la uchomaji mali kwa makusudi ambalo liliharibu gari aina ya Porsche, baiskeli ya miguu minne na mali zenye thamani ya Pauni za Uingereza 22,000.
Wakati wa utumishi wake kama mkuu wa manispaa ya Mbombela mjini Mpumalanga aliwahi kulazwa hospitali mara tatu kwa msongo na kila mara alikuwa katika vita na mwenyekiti wa Chama cha African National Congress.
Udhaifu wake wa akili iliripotiwa kupunguzwa na mauaji ya mwanasiasa mwenzake aliyempiga risasi na kumuua wakati akijiandaa kulipua skendo ya rushwa mwaka 2009.
Clayson Monyela, msemaji wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano (DIRCO), alithibitisha kwamba Chiwayo amerejeshwa nyumbani 'kwa sababu za kiafya'.
"Anapatiwa msaada kutoka kwenye Idara hiyo," alisema Monyela.

No comments: