Msichana mwenye umri chini ya miaka 20 alibakwa mara 90 katika wikiendi moja imebainishwa, kwenye ripoti ya kushitusha katika zama za utumwa mamboleo nchini Uingereza.
Ripoti hiyo, inayotarajiwa kuchapishwa leo na Kituo cha Haki za Jamii, imejumuisha ushahidi kutoka kwa msichana huyo, ambaye alikuwa na miaka 16 wakati huo alipchukuliwa utumwani na kubakwa na wanaume 90.
Msichana huyo, ambaye alitoa ushahidi kwa tume hiyo licha ya kuendelea kuwa "ameathirika" kwa mashambulio hayo, hakuelezea historia yake iliyosababisha kuingia katika hatari hiyo, lakini akawa mtumwa baada ya kuwa rafiki na wasichana wasio salama kuweza kudhuriwa, imeripotiwa.
Andrew Wallis, mwenyekiti wa kundi lililoshughulika na ripoti hiyo, aliweza kuieleza tume hiyo msichana huyo 'kwa sasa yuko salama' alipoulizwa kilichomtokea tangu mashambulio hayo, kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times.
Ripoti hiyo inadai juhudi za kupambana na utumwa mamboleo katika Uingereza, ikiwamo udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto, umefikia hatua ya kuwa janga kubwa.
Tume hiyo, imeishambulia serikali kwa 'uzito wake kushughulikia' tatizo hilo baada ya uchunguzi kubaini usafirishaji haramu wa binadamu.
Utafiti wake umegundua zaidi ya watu wazima 1,000 na watoto walisafirishwa kuingia au ndani ya ya Uingereza mwaka 2011/2012.
Wanaume tisa kutoka Asia walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka minne na 19 mwaka jana kwa kuwaweka kinyumba wasichana wa Kizungu ndani na kuzunguka mji wa Rochdale.
Wanaume hao waliwachukua kutoka mageti ya shule na kuwapeleka kwenye nyumba na maghorofa kuwanywesha pombe na dawa za kulevya kabla ya kufanya nao mapenzi kwa kupokezana.
Watoto 47 walitambuliwa kama waathirika wa udhalilishaji huo ambao umewaacha wengi maisha yao kuwa katika matatizo.
Wasichana wote walikuwa wakihongwa ili wanyamaze kuhusu udhalilishaji huo kupitia pombe za bure na dawa za kulevya, chakula, kiasi kidogo cha pesa na zawadi nyingine.
Ingawa baadhi ya waathirika walifanya mapenzi kwa ridhaa yao na wadhalilishaji hao, wengine walikuwa wakishambuliwa mwilini na kubakwa na hadi wanaume watano kwa mara moja.

No comments:
Post a Comment