Seti ya Televisheni inayotumia mfumo wa digitali. |
Wamiliki wa vituo vya televisheni nchini, wameiomba Serikali kurudisha mfumo wa analojia, uendeshwe sambamba na wa digitali, ili kurudishia wananchi haki yao ya kupata habari.
Wamehadharisha, kwamba endapo mfumo wa digitali utaachwa uendelee ndani ya miezi miwili au mitatu ijayo, vyombo vya televisheni vitashindwa kuendeshwa kwa kukosa matangazo na kufungwa.
Akizungumza jana Dar es Salaam, mmoja wa wamiliki hao, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, alisema hali ya vyombo vya televisheni nchini si nzuri kutokana na mabadiliko hayo.
Mengi alisema waliamini kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeliona hilo na ingelifanyia kazi, kama ambavyo wamekuwa wakitoa malalamiko yao katika vikao visivyo rasmi.
Alisema hatua ya kuhamia kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali, imekuwa na matatizo makubwa na kinachosikitisha zaidi ni mfumo huo kufanywa kwa haraka, huku wananchi wengi wakikosa haki ya kupata habari kutokana na kukosa ving'amuzi huku televisheni zikikosa matangazo.
"Sijui Tanzania ilidhani itafanya maajabu gani ya kuhama haraka namna hiyo? Marekani ilichukua miaka 11, Uingereza 14, Hispania 10 na Japan minane, nchi nyingine zilitoa vocha kwa kila kaya kwa ajili ya kununulia ving'amuzi," alisema Mengi na kuongeza kuwa Tanzania haina chochote ilichofanya kwa wananchi wake.
"Mlalahoi uwezo wa kulipia king'amuzi ni tatizo, amenyimwa haki yake ya kupata habari kikatiba ... ni vizuri sana kuhama kwenda digitali, lakini Serikali ingesaidia wananchi walio wengi ambao ni walalahoi kwa kuwekeza kununua ving'amuzi kabla ya mfumo huo kuanza," alisema na kuongeza kuwa kwa sasa ni vema mifumo hiyo ikaenda pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Sahara Communications, Samwel Nyala alisema Tanzania imefanya haraka kuhamia mfumo wa digitali, tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki, jambo ambalo sasa limewageukia wamiliki wa televisheni kwa kukosa matangazo.
"Tangu kuanza kwa mfumo wa digitali, wenye matangazo waliyaondoa katika televisheni kutokana na kutoonekana kwa walengwa. Jambo hili limesababisha tushindwe kuendesha vyombo hivi huku mikoa mingine ikiwa haina haki ya kupata habari," alisema Nyala.
Meneja wa Media Group, Ruge Mutahaba, alisema kukosekana kwa ving’amuzi kwa Watanzania wengi, kumesababisha wananchi wengi wafikie mahali ambapo wamezoea kutopata habari na kuwanyima haki yao ya msingi.
Alisema kuhamia mfumo wa digitali, kumewatenga wananchi na kwamba ipo mikoa mingine ambayo itashindwa kabisa kupata haki hiyo kutokana na mfumo huo kuwatenga.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alisema kuhamia digitali hakukufanywa kwa haraka, kwani mchakato ulianza tangu mwaka 2006 na ulikuwa ukishirikisha wadau.
“Hakuna kurudi nyuma, mwendo ni mbele kwa mbele…changamoto zilizopo zitatatuliwa kadri muda unavyosogea na ndio maana haijazimwa mikoa yote,” alisema.

No comments:
Post a Comment