CHEKA TARATIBU...

Mlevi mmoja alikuwa akitembea kando ya mto akamwona Mchungaji anawabatiza watu. Na yeye akaingia kwenye maji na kupanga poleni. Ikafika zamu yake, Mchungaji akamzamisha kichwa kwenye maji na kumuuliza: "Umempokea Yesu?" Mlevi akajibu: "Hapana". Mchungaji akamzamisha tena kwenye maji na kuuliza: "Umempokea Yesu?" Mlevi akajibu: "Hapana". Mchungaji akamzamisha kwa mara ya tatu na kuuliza: "Umempokea Yesu?" Mlevi kwa ukali akajibu: "Hivi una uhakika alizama hapa?" Balaa...

No comments: