Madereva wawili na utingo wamekufa papo hapo kwa kuteketea kwa moto baada ya magari yao kugongana uso kwa uso na kulipuka mkoani Tanga.
Tukio hilo ni la juzi saa 1:45 usiku katika barabara kuu ya Tanga –Segera, eneo la Kilapura ‘A’ lililoko umbali wa kilometa 15 kutoka katikati ya jiji la Tanga kwenda wilayani Muheza.
Wakazi wa Kata ya Pongwe na vitongoji vyake walioshuhudia tukio hilo, wanasema walishindwa kuokoa watu hao waliokuwa wamebanwa ndani ya vichwa vya malori hayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, magari sanjari na miili ya watu hao, iliendelea kuteketea kwa takribani saa mbili kabla ya moto kuzimwa. Majina ya madereva yalipatikana wakati la utingo halikupatikana mara moja.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alitaja magari yaliyohusika ni aina ya Scania lenye namba T 134 AEX na tela namba T 389 AJH lililokuwa likiendeshwa na Ali Joba akitoka jijini Tanga kwenda wilayani Muheza.
Gari lingine lilikuwa na namba za usajili T 524 ALG na tela lenye namba T 102 AYF lililokuwa likiendeshwa na Rajabu Ramadhan kutoka Muheza kwenda Tanga.
Kamanda alisema wakati magari hayo yakikaribia eneo la Kilapura A, gari lililokuwa likiendeshwa na Joba ndilo lilitangulia na kukuta ajali ndogo ya pikipiki iliyogonga baiskeli na kwamba wahusika walikuwa wakizozana katikati ya barabara.
“Kwa kuwa ilikuwa ghafla, dereva wa lori kutoka Tanga aliamua kuwakwepa na kujaribu kuingia upande wa kushoto wa barabara ambako ndiko alikutana na lori kutoka Muheza na kugongana uso kwa uso kisha yakashika moto mkubwa kuanzia kwenye bodi,” alisema.
Alisema chanzo cha ajali ni mwendo wa kasi waliokuwa nao maderava wa magari hayo hivyo baada ya kubaini ajali ndogo ya pikipiki na baiskeli, walishindwa kufunga breki kupunguza mwendo na kusimama.
“Katika hili niendelee kutoa mwito kwa madereva na watumiaji wote wa barabara kuhakikisha wanakuwa makini wakati wote na kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti au kusubiri kumuona askari wa usalama barabarani,” alisema.
Wakati huo huo, ajali hiyo ilisababisha adha kwa wasafiri katika barabara hiyo hali iliyolazimu wasafirishaji wa pikipiki na daladala zinazofanya safari zake kati ya Pongwe na Tanga kufanya kazi ya kusafirisha abiria.
Magari yalianza safari kupita eneo hilo la tukio saa 5 usiku. Kazi ya uzimaji wa moto ambao uliteketeza miili hiyo ilifanywa kwa ushirikiano wa wananchi na maofisa wa kikosi cha Zimamoto na Ukokoaji jijini humo.

No comments:
Post a Comment