BINTI ABAKWA NDANI YA BASI AKITOKA 'SHOPINGI'...

Binti huyo alikuwa akitokea kwenye maduka haya.
Msichana mdogo amebakwa na wanaume wawili kwenye sehemu ya juu ya basi baada ya kutoka kwenye eneo lenye maduka mengi akiwa na rafiki yake.

Msichana huyo mwenye miaka 14 alishambuliwa kwenye sehemu ya juu ya basi namba 57 wakati akitoka kwenye maduka ya Silverburn yaliyoko Pollok, mjini Glasgow.
Pale wasichana hao walipopanda kwenye basi hilo, waliketi kwenye viti sehemu ya chini. Muathirika huyo alihamia sehemu ya juu ambako aliingia kwenye majibizano na wanaume wawili ambao walipanda basi hilo katikati ya jiji.
Kisha baadaye akashambuliwa na kubakwa na wote wawili. Rafiki yake, ambaye pia ana miaka 14, alipandisha juu kumwangalia na kutoa taarifa kwa abiria waliokuwa sehemu ya chini.
Mwanamke mmoja na wanaume wawili walikwenda kuwasaidia wasichana hao. Wote walishuka kwenye basi hilo vituo viwili vilivyofuata kutoka Silverburn.
Abiria hao inasemekana walisubiria pamoja nao hadi walipopata basi jingine kuelekea nyumbani, inakodhaniwa kuwa ni eneo la Darnley jijini humo, ambako polisi walitaarifiwa.
Tukio hilo lilitokea majira ya Saa 4:30 usiku wa Ijumaa ya Machi 22, mwaka huu.
Hakuna picha yoyote ya kamera za CCTV iliyopatikana kutoka kwenye basi hilo wakati polisi wa Strathclyde wakiwataka abiria wote kujitokeza kusaidia uchunguzi wao.
Washambuliaji hao wote wanasemekana kuwa na umri wa kati ya miaka 18 na 20. Mmoja ana urefu wa takribani futi 5 na inchi 10, akiwa amenyoa nywele kichwani huku akiwa kavalia sweta lenye kofia.
Mwanaume mwingine ana nywele za kahawia zilizochingoka na alikuwa kavalia suti ya mazoezi inayowezekana kuwa ya kijivu, na jaketi la kutunza joto mwilini.
Mkuu wa Upelelezi, Jackie Caroll, kutoka Greater Glasgow CID, alisema: "Hii ilikuwa changamoto ya kuogofya kwa msichana mdogo aliyehusika na, shukrani, alisaidiwa na rafiki yake na wasamaria katika basi hilo ambao walihakikisha anafika nyumbani salama.
"Ameachwa akiwa na maumivu kufuatia mateso yake hayo. Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo na tuwatafuta wanaume wawili na mwanamke ambao walikwenda kumsaidia kutokana na kuwa na taarifa muhimu ambazo zinaweza kutusaidia katika uchunguzi.
"Tunafahamu kwamba wanaume hao waliohusika walipanda basi hilo katikati ya jiji. Wanaume hao walikuwa na kelele na kutumia lugha chafu kwa abiria wengine.
"Dereva wa basi hilo aliwashusha wanaume hao wawili kutoka kwenye basi hilo kwenye kituo cha Pollokshaws Road (karibu na Queen’s Park) majira ya Saa 6.30 usiku.
"Napenda kuongea na kila mtu ambaye alikuwapo kwenye basi wakati wa shambulio hilo, ili kutuwezesha kuwakamata watu hawa."
Msemaji wa First Glasgow alisema dereva wa basi hilo hakushuhudia tukio hilo.
Alisema: "Tunaisaidia polisi katika uchunguzi wao na tunatangaza ombi lao kwa yeyote kujitokeza ambaye ana taarifa zozote kuhusu tukio hilo.
Dereva wetu hakufahamu chochote kuhusu shambulio hilo. Kwa bahati mbaya, tukio hilo lilitokea sehemu ya juu ya basi na hivyo mbali na upeo wa macho ya dereva na hakuna yeyote ndani ya basi hilo aliyemfuata dereva kuripoti usumbufu wowote.
"Dereva aliwashusha wanaume wawili muda fulani baadaye katika safari hiyo - hii ni kutokana na tabia zao chafu zisizovumilika.
"Usalama na ulinzi wa wafanyakazi wetu na abiria ni kipaumbele cha kwanza na tutaendelea kuvanya kila kitu tunachoweza kusaidia polisi kuwatia mbaroni wahusika hao."
"Tunaungana na muathirika wa shambulio hilo," aliongeza.

No comments: