ZEE LA MIAKA 60 LAZABA KIBAO USONI KATOTO KA MIEZI 19 KWENYE NDEGE...

JUU: Joe Rickey Hundley. CHINI: Jonah. KULIA: Ndani ya ndege ya Delta ambako tukio hilo lilifanyika.
Mtu mmoja anadaiwa kumtolea maneno ya kibaguzi kisha kumshambulia mtoto wa miezi 19 kwenye ndege iliyokuwa ikielekea Atlanta mwishoni mwa wiki iliyopita.
Joe Rickey Hundley, mwenye miaka 60, anadaiwa kutaka mama huyo wa mtoto aliyekuwa akilia "kukanyamazisha haraka" kabla ya kuzaba kibao usoni ndani ya ndege ya Delta.
Kwa mujibu wa gazeti la The Smoking Gun, Hundley ameshitakiwa kwa shambulio rahisi baada ya tukio dhidi ya Jessica Bennett, mwenye miaka 33, na mtoto wake wa  kiume, Jonah.
Bennett alizieleza mamlaka kwamba mtoto wake 'alianza kulia kufuatia mabadiliko ya mwinuko kutoka usawa wa bahari' wakati ndege hiyo kutoka Minneapolis kwenda Atlanta ikijiandaa kutua.
Jessica na mtoto wake aliyemuasili walichangia kiti kwenye safari yao kwenda kwenye msiba wa familia wakati Hundley alikuwa katika kiti cha jirani.
Bennett alisema hakuwa na uwezo wa kumnyamazisha mtoto huyo aliyekuwa akilia. Ripoti iliyoandaliwa na wakala wa FBI Daron Cheney ilidai kwamba Hundley alimgeukia mama huyo na kutumia lugha ya kibaguzi kumweleza amnyamazishe mtoto huyo.
Kama ilivyoripotiwa na gazeti la The Smoking Gun, Hundley kisha 'akazunguka na kunasa kibao' mtoto huyo mchanga usoni, "jambo lililomfanya muathirika huyo kupiga kelele kwa sauti kubwa zaidi." Kwa mujibu wa mama huyo, kibao hicho 'kilisababisha mkwaruzo chini ya jicho la kulia la mtoto huyo.'
Hundley alishitakiwa kwa shambulio rahisi kwenye mahakama mjini Atlanta. Kama atatiwa hatiani mtu huyo atakabiliwa na kifungo kisichozidi mwaka mmoja jela.
Mtu huyo mwenye miaka 60, ambaye ni rais wa kiwanda cha kutengeneza vipuri vya ndege chenye makao yake mjini Idaho, alikana kumzaba kibao mtoto huyo au kutumia maneno ya kibaguzi. Anadai kwamba 'alimwomba mama huyo kumnyamazisha mtoto wake.'
Hundley alisema alikuwa akisafiri kwenda Atlanta kumtembelea jamaa yake aliyelazwa hospitali, akifafanua hali ya mhemuko wake kuwa 'alichanganyikiwa' na kwamba alikuwa amekunywa chupa moja ya pombe kwenye ndege hiyo.
Hatahivyo, Jessica alilieleza gazeti la The Smoking Gun kwamba anaamini Hundley alikuwa amelewa. Mama huyo alisema kwamba 'alikuwa akinuka pombe', na kwamba alikuwa akinunua vodka mfululizo wakati wote wa safari.
Jessica anasema Hundley alimweleza kwamba Jonah alikuwa mkubwa vya kutosha kuwa 'mtoto wa kupakatwa.'
Wakala Cheney aliongeza kwamba Bennett alipata msaada kutoka kwa abiria wengine kwenye ndege hiyo ya Delta. Todd Wooten, ambaye alikuwa ameketi mstari wa 12 mbele, alizieleza mamlaka kwamba 'alisikia lugha ya kushusha heshima ikitokea nyuma ya ndege hiyo' na kwenda kujionea kilichokuwa kikiendelea.
"Kwa mujibu wa Todd," Cheney aliandika, 'alimwona Joe Rickey Hundley akimshambulia' mtoto huyo.
Hundley alipatikana na hatia kwa kosa dogo la shambulio kwenye mahakama ya Virginia mwaka 2007 baada ya kuwa amekamatwa kufuatia kukwaruzana na rafiki yake wa kike.
Kwanza alishitakiwa kwa shambulio rahisi, kubeba silaha iliyofichwa, na kulewa hadharani.
Hundley alilieleza gazeti la The Smoking Gun kwamba silaha hiyo aliyodaiwa kubeba ilikuwa ni kizibuo.

No comments: