NDEGE YA EMIRATES YATOBOKA MLANGONI IKIWA UMBALI WA FUTI 27,000 JUU...

Mtalii wa Uingereza alieleza juzi kuhusu ugaidi katika ndege yake pale alipodai mlango wa dharura kwenye ndege aina ya super jumbo ulipopigwa kishindo na kufunguka wakati ndege hiyo ikiwa umbali wa futi 27,000 angani.
David Reid na mtoto wake wa kiume, Lewis walihofia bomu limelipuka mahali hapo baada ya kusikia 'mlipuko mkubwa' masaa mawili katika safari yao kwenye ndege hiyo mpya kabisa ya Emirates Airbus A380 yenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 250.
Hewa yenye barafu iliingia ndani na mgandamizo wa hewa ukatumbukia ndani baada ya mlango huo katika daraja la kati kufunguka kidogo kwa inchi moja na nusu, kuacha tundu la wazi, alisema David.
Huku abiria wakilia ugaidi, alisema, mhudumu aliyeotishwa mno alikimbia ghorofa ya chini na kupiga mayowe "mlango unang'oka" kabla ya kujibanza nyuma ya kiti chake.
Mkasa huo ulitokea Jumatatu iliyopita ambapo Waingereza wawili walisafiri kwa ndege hiyo kutoka Bankok kwenda Hong Kong kama sehemu ya kile walichopanga kama "safari ya aina yake maishani".
Alisema: "Tulikuwa humo kama masa mawili ndipo ghafla kukatokea mlipuko mkubwa.
"Hakika ulikuwa mshituko mkubwa, kwa sauti kubwa kwamba nilifikiri bomu limelipuka. Hewa wilikuwa ikiingia kwa kasi ndani kama dhoruba.
"Mhudumu wa kike akaruka na kukodolea macho mlango. Uso wake ulinyonya unyevu mweupe.
"Alikimbia baina ya viti, akanyakua simu ya ndani na kuanza kupiga mayowe, "Mlango unaelekea kung'oka, mlango unaelekea kung'oka!" Kisha akajificha chini ya kiti chake.
"Abiria wengine walikuwa wakilia na kusema "Tunaelekea kuanguka chini, tunaelekea kuanguka chini."
"Ilikuwa ni hofu kubwa. Mlango huo wa dharura ulikuwa wazi kidogo na kuacha tundu. Ungeweza kuona moja kwa moja mazingira, futi 27,000 juu."
David, ambaye ana leseni ya rubani wa kujitegemea, alisema kwamba baada ya matukio kadhaa ya kuchanganyikiwa, mhudumu huyo wa ndege akaanza kuvuta mablanketi na mito ambayo ilifungwa pamoja kwa gundi ya nailoni kuziba uwazi huo.
Aliongeza: "Huu ni ubunifu wa ndege lakini walikuwa wakitumia njia chafu zaidi unayoweza kudhani kujaribu na kuziba tundu hilo.
"Hali ilikuwa ya kuogofya kwa wengine waliobaki katika ndege hiyo. Mlango uliendelea kutoa mlio wa mkubwa ajabu ambao ulifanya iwe vigumu kuongea na mwenzako.
"Mbaya zaidi, tulikuwa tukikaribia kuganda kwa baridi."
Alisema mhudumu wa daraja hilo alifunga pazia linalotenganisha daraja la kati kuzuia wale wote walio sehemu ya daraja la kawaida wasigundue kilichokuwa kikiendelea.
David alidai alimepata madhara ya kifua kufuatia mateso hayo na wawili hao walilazimika kufupisha safari yao kwa Pauni za Uingereza 4,500.
Mtoto wake wa kiume mwenye miaka 18 aliripoti tukio hilo kwa Tawi la Uchunguzi wa Ajali za Anga la Idara ya Uchukuzi ambao walipeleka kwa wachunguzi wa anga katika Mamlaka Kuu ya Usafiri wa Anga ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
Msemaji wa Emirates alisema: "Tunathibitisha kulikuwa na kelele kutoka kwenye moja ya milango katika A380 deki ya juu katika ndege namba EK384 kati ya Bankok na Hong Kong Jumatatu, Februari 11. Usalama wa ndege hiyo ukawa katika hatihati."
Msemaji wa Airbus alisema: "Haiwezekani kwa mlango sehemu ya abiria kufunguka katika A380 au katika ndege yoyote wakati ikiwa angani, maana milango inafunguka kwa kuelekea ndani na huwa inajifunga yenyewe."

No comments: