MSICHANA WA MIAKA 17 ABAKWA NA KUNDI LA WAHUNI NA KUKATWA VIUNGO...

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Anene Booysen tayari kwa mazishi.
Mauaji ya kutisha ya msichana wa miaka 17, ambaye alibakwa na genge la wahuni, kukatwa viungo na kutelekezwa akikata roho kwenye kiwanja cha jengo, yamelipua kilio kwa taifa zima nchini Afrika Kusini.
Anene Booysen aligunduliwa na walinzi kwenye kiwanja hicho katika mji wa Bredasdorp, maili 80 mashariki mwa Cape Town.
Kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Afya, majeraha yake yalikuwa makubwa  kiasi kwamba familia yake kutaka mamlaka zisitoe taarifa zake.
Hatahivyo ilibainika baadaye kwamba tumbo lake lilikuwa limechanwa kabisa hadi kwenye sehemu za siri na kwamba alikufa kutokana na majeraha yake kwenye hospitali.
Alifanikiwa kumtambua mmoja wa waliomshambulia kabla ya kifo chake na wanaume wawili wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya ubakaji na mauaji.
Hakimu aliamuru wawili hao, ambao walificha sura zao mbele ya kamera za televisheni na wapigapicha mahakamani, kubaki rumande hadi Februari 26 wakati maombi ya dhamana yatakaposikilizwa. Watuhumiwa hao wanakabiliwa na kifungo cha maisha endapo watapatikana na hatia.
Polisi walimwachia mtu wa tatu aliyekamatwa baada ya tukio kufuatia kukosekana kwa ushahidi unaomhusisha na uhalifu huo, lakini walisema walikuwa wakichunguza endapo kuna wengine walihusika.
Umati wa watu 100 uliandamana nje ya jengo la mahakama mjini Bredasdorp, wakiwa wamebeba mabango yanayosema "Hakuna huruma kwa wabakaji" na "Hakuna dhamana kwa wauaji".
Kaka wa Booysen alivieleza vyombo vya habari vya mjini humo alimfahamu mmoja wa watuhumiwa.
Alisema: "Alikuwa rafiki yangu, tulikwenda shule pamoja, kuishi kwenye nyumba moja, tulikuwa kama ndugu."
Ijumaa, mamia ya watu waliandamana hadi Bredasdorp, wakiimba "imetosha" na mamia walihudhuria mazishi yaliyofanyika Jumamosi.
Mamia ya waombolezaji, wakiwamo wanasiasa, walijaza kanisa katika mji wa Bredasdorp, wakati turubai liliwekwa kwa ajili ya wote ambao hawakupata nafasi ndani.
Mauaji hayo yamekumbushia kubakwa kwa mwanafunzi ndani ya basi mjini New Delhi mwaka jana, na kumulika kwa umakini viwango vya juu vya uhalifu wa ubakaji katika Afrika Kusini.
Booysen alikutwa na walinzi akiwa amelala umbali mfupi kutoka nyumbani kwake baada ya kuwa kwenye sherehe katika baa jioni ya Ijumaa iliyopita.
Umoja wa Wanawake wa chama tawala cha African National Congress unajaribu kuhamasisha jamii kuchukua hatua kama hiyo ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambayo imefanyika nchini India baada ya shambulio hilo la New Delhi.
Jumamosi, vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti polisi wamemkamata mchungaji wa Johannesburg kwa kumshawishi mwanamke ndani ya kanisa lake na kumbaka.
Rais Jacob Zuma alielezea mshituko wake na kufedheheka, akitaka adhabu kali iwezekanavyo kwa wauaji na kuchochea kampeni 'kukomesha njia hii ya ulipizaji kisasi katika jamii yetu'.
Waziri wa Wanawake wa Afrika Kusini alitaka Jumanne nguvu zaidi itumike.
Waziri wa Wanawake, Lului Xingwana, ambaye amekutana na familia ya muathirika huyo alisema: "Tunasema kwa mahakama leo kusiwepo na dhamana kwa wahalifu hawa na wanyama."
"Tunatarajia hukumu kali na ya kutisha ambayo inaweza kuwa fundisho kwa wahalifu wengine ambao unadhalilisha na kuua wanawake wetu na watoto."
"Kama mwanaharakati ninashinikiza kwa nguvu zote kwamba kusiwe na dhamana kwa hawa wanyama. Wangefanya nini kama hili lingetokea kwa mwanafamilia wao yeyote?" alisema Faraah September.
Afrika Kusini ina idadi kubwa ya matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa huku zaidi ya 64,500 yakiripotiwa katika kipindi cha 2011/2012.
Ubakaji unasemekana kufanyika nchini Afrika Kusini kila baada ya dakika nne.

No comments: