Askari akimfungua pingu Shekhe Ponda Issa Ponda. |
Upande wa Utetezi katika kesi ya uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Sh milioni 59 umeandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kulalamikia kitendo cha kuwanyima dhamana viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shehe Issa Ponda na Mukadam Swalehe.
Wakili wa Utetezi, Juma Nassoro alidai hayo jana nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi hiyo inayowakabili viongozi hao na wafuasi 48 kuahirishwa.
Alisema wamewasilisha barua hiyo yenye kumbukumbu namba RJ/CC/245/2012 Desemba 24 mwaka jana, kulalamikia kitendo cha DPP kuwanyima dhamana Shekhe Ponda na Mukadam kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yanafanana na yanayowakabili washitakiwa wengine.
Nassoro alidai kuwa, kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka mpaka sasa hakuna shahidi hata mmoja ambaye ameeleza kuwa washitakiwa hao walisababisha uvunjifu wa amani.
Hata hivyo, Mahakama imetoa hati ya kukamatwa kwa shahidi wa upande wa mashitaka kwa kosa la kuidharau Mahakama kwa kutofika kutoa ushahidi bila taarifa.
Awali Wakili wa Serikali Tumaini Kweka aliomba ahirisho fupi kwa kuwa mashahidi waliotakiwa kutoa ushahidi jana hawakufika mahakamani na kuongeza kuwa shahidi mmoja anaumwa mwingine amesafiri lakini watatu alipokea hati ya kuitwa mahakamani akasaini na hajafika bila kutoa taarifa.
Hakimu Victoria Nongwa alisema ameona hati ya kuitwa mahakamani iliyosainiwa na shahidi huyo hivyo mahakama imetoa hati ya kukamatwa kwa shahidi huyo ambaye Wakili Kweka hakutaka kumtaja kwa sababu za kiusalama.
Wakili Nassoro alidai kuwa hiyo siyo sahihi na ni ngumu kuamini kwa sababu mwanzo walidai wana mashahidi zaidi ya 40 kwa nini kama hao hawajapatikana wasilete mashahidi wengine. Pia alilalamikia kitendo cha Wakili huyo kutotaja majina ya mashahidi.
Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hado Januari 14 mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya Shekhe Ponda na Mukadam ambao wapo rumande na DPP amezuia dhamana yao. Kesi itaendelea kusikilizwa Januari 17.
Shekhe Ponda na wenzake 49 wanakabiliwa na mashitaka matano ambapo Oktoba 12 mwaka jana, katika eneo la Chang’ombe Markazi washitakiwa walipanga njama za kuingia kwenye kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agri Tanzania Ltd kwa nia ya kujimilikisha kiwanja hicho isivyo halali.
Aidha inadaiwa kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka jana huko Chang’ombe Markazi pasipo na uhalali, washitakiwa wote katika hali iliyokuwa ikipelekea uvunjifu wa amani waliingia na kujimilikisha kwa nguvu ardhi ya kampuni hiyo na kuiba mali zenye thamani ya Sh milioni 59.7.
Katika shitaka la uchochezi linalowakabili Shekhe Ponda na Swalehe, inadaiwa katika eneo hilo la Chang’ombe Markazi kwa maelezo kuwa wao ni viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu waliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao kutenda makosa hayo.

No comments:
Post a Comment