Mkazi wa kijiji cha Miangalua wilayani hapa, Juliana Moche (28) anadaiwa kumpiga na kumuua mumewe Johan Ismail (35) akimtuhumu kumwibia mahindi yenye thamani ya Sh 4,000 na kuyauza na kutumia fedha zote ulevini.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha jana kutokea kwa mauaji hayo kwa maelezo kuwa chanzo ni ugomvi baina ya wanandoa hao.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Mwaruanda alidai kuwa Desemba 29, Juliana alikwenda kufanya kibarua cha kulima mashamba ya wanakijiji wenzake na kupata ujira wa Sh 4,000.
“Baada ya kulipwa ujira huo, alinunua kilo 10 za mahindi kwa fedha hizo na kuyahifadhi nyumbani ili kesho yake akasagishe unga kwa ajili ya kula familia hiyo yenye watoto wanne.
“Lakini mumewe aliporudi nyumbani jioni alichukua mahindi hayo na kuyauza na fedha zote kunywea pombe,” alisema Kamanda.
Kwa mujibu wa Kamanda, mume huyo anayefahamika zaidi kama Pandisha, alirejea nyumbani amelewa na kusababisha ugomvi na mkewe hata kupigana.
Wakati wakipigana kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, mkewe alitumia kitu chenye ncha kali kumpiga mumewe kichwani na kusababisha avuje damu nyingi na kufariki dunia Desemaba 30 asubuhi.
Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.

No comments:
Post a Comment